Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

ZIFAHAMU AINA MBILI ZA KISUKARI yaani Diabetes Type 1 and Diabetes Type 2

 KISUKARI

• • • • • •

ZIFAHAMU AINA MBILI ZA KISUKARI yaani Diabetes Type 1 and Diabetes Type 2


DIABETES TYPE 1


Hii ni aina ya kisukari ambayo hutokana na Kongosho au Pancrease kuzalisha kiwango kidogo sana cha INSULIN au kutokuzalisha kabsa.


– Aina hii ya kisukari kwa asilimia kubwa huwapata sana Watoto pamoja na Vijana


DALILI ZA AINA HII YA KISUKARI(DIABETES TYPE 1)


– Mgonjwa kuona marue rue


– Mwili kuchoka kupita kiasi na kuwa dhaifu sana


– Uzito wa mwili kupungua kwa kasi sana na mtu kukonda


– Mtu kuhisi njaa sana kila mara


– Mtoto kuanza kujikojolea kitandani wakati wa usiku wakati hakuwa na shida hyo hapo mwanzo kabla ya ugonjwa


– Kukojoa mara kwa mara


– Mtu kupata kiu sana ya maji



KUMBUKA; hakuna tiba ya aina hii ya kisukari bali kuna matibabu dhidi ya kudhibiti dalili zake pamoja na kiwango cha sukari kwenye damu


DIABETES TYPE 2


– Hii ni aina ya kisukari ambayo hutokea baada ya mwili kushindwa kudhibiti,kurekebisha na kutumia sukari iliyopo hali ambayo hupelekea kiwango kikubwa sana cha sukari kuwepo kwenye damu,


na shida hii hutokea pale ambapo, Kongosho au Pancrease haizalishi kiwango cha kutosha cha Insulin au Hormones ambazo hurekebisha kiwango cha sukari ndani ya seli kutokufanya kazi vizuri na Insulin hivo kupelekea kiwango kidogo sana cha Sukari kuchukuliwa na Seli.


– Aina hii ya kisukari huwapata sana Watu wazima kuliko watoto na vijana


KUMBUKA; hakuna tiba ya aina hii ya kisukari bali kuna matibabu dhidi ya kudhibiti dalili zake pamoja na kiwango cha sukari kwenye damu



DALILI ZA AINA HII YA KISUKARI(DIABETES TYPE 2)


✓ Vidonda kuchelewa sana Kupona


✓ Mtu kupata kiu sana


✓ Kukojoa mara kwa mara


✓ Kupata njaa sana kila mara


✓ Uzito wa mwili kushuka kwa kasi


✓ Mwili kuchoka kupita kawaida


✓ Kuona marue rue


✓ Kupata maambukizi ya magonjwa ya mara kwa mara


✓ Kuhisi hali ya kuchomwa chomwa kwenye miguu na mikono



ZINGATIA HAYA;


– Hakikisha unapata dawa kama Insulin therapy n.k


– Kufanya mazoezi kila siku angalau dakika 30 au nusu saa


– Kula vyakula ambavyo vina virutubisho vyote


-N.k



KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.


Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.