Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

TATIZO LA NGOZI KUWA KAVU,KUPAUKA NA KUPASUKA

 NGOZI

• • • • • •

TATIZO LA NGOZI KUWA KAVU,KUPAUKA NA KUPASUKA


Tatizo la ngozi kuwa kavu,kupauka na kupasuka huweza kuonekana maeneo mbali mbali ya mwili kama vile kwenye mikono,miguuni n.k, Hata hivo tatizo hili huweza kuwa la muda mfupi au muda mrefu kwa baadhi ya watu kulingana na hali ilivyo kama vile uwepo wa magonjwa ya ngozi,umri,hali ya hewa n.k


CHANZO CHA TATIZO LA NGOZI KUWA KAVU,KUPAUKA NA KUPASUKA


1. Hali ya hewa, baadhi ya watu huanza kupata tatizo hili la ngozi kuwa kavu,kupauka au kupasuka wakati wa Baridi sana na baadhi yao baada ya kuchomwa na jua kali au joto kali


Hapa asilimia kubwa ya watu wenye tatizo la ngozi kuwa kavu,kupauka au kupasuka wakati wa hali ya hewa kama vile; baridi kali huweza kupona tu kwa kutumia mafuta mbali mbali ya kulainisha ngozi ya mwili kwa kipindi hiki


2. Tatizo la ngozi ya mwili kuunguzwa na vyanzo mbali mbali vya joto kali kama vile moto wenyewe(wale wanaokaa sana jikoni),jua n.k


3. Tabia ya kuoga na maji ya moto kwa muda mrefu na mara kwa mara hasa kwa wale wanaopenda kuoga kwenye swimming pool za maji ya moto huweza kusababisha ukavu kwenye ngozi ya mwili


4. Kuwa na magonjwa mbali mbali ya ngozi kama vile Atopic dermatitis au Eczema


5. Matumizi ya baadhi ya sabuni za kuogea zenye kemikali kali huweza kuondoa layer ya mafuta kwenye ngozi na kuleta tatizo la ngozi kuwa kavu,kupauka na kupasuka pia.


DALILI ZA TATIZO HILI LA NGOZI KUWA KAVU,KUPAUKA NA KUPASUKA NI PAMOJA NA;


– Mtu kuhisi ngozi kukakamaa isivyo kawaida hasa baada ya kutoka kuoga


– Ngozi ya mwili kuaza kuwa na mikwaruzo hasa maeneo ya miguuni na kwenye mikono


– Ngozi ya mwili kuanza kuwasha mara kwa mara


– Ngozi ya mwili kuanza kutoka magamba kidogo kidogo pamoja na unga mweupe


– Ngozi ya mwili kuwa na kreki hasa maeneo ya miguuni na mikononi


– Ngozi ya mwili kuanza kubadilika rangi na kuwa kijivu,dhambarau au nyekundu zaidi


– Na kwa baadhi ya watu ngozi ya mwili hupasuka au kuwa na kreki hadi kupelekea damu kuvuja


– Ngozi ya mwili kuchubuka yenyewe


UKIONA DALILI HIZI HAPA CHINI MUONE DAKTARI MAPEMA ZAIDI


• Ngozi kuwa kavu hadi kuwa nyekundu au kuvuja damu


• Ngozi kuwa kavu na kuwasha hadi kupelekea mtu kushindwa kulala usiku


• Ngozi ya mwili kuchubuka kwa kiwango kikubwa zaidi


• Kuanza kupata vidonda kwenye ngozi yako

N.k


WATU AMBAO WAPO KWENYE HATARI YA KUPATWA NA TATIZO HILI NI PAMOJA NA;


✓ Wenye umri wa kuanzia miaka 40 na kuendelea


✓ Wanaoshi maeneo yenye baridi sana pamoja na hali ya hewa kavu


✓ Wanaofanya kazi ambazo huhitaji kushika maji mara kwa mara


✓ Wanaopenda kuoga kwenye swimming pool za maji ya moto N.k


KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.



Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.