Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

TATIZO LA KUUMWA UBAVU WA KUSHOTO WAKATI WA KULALA

Kuna wakati maumivu haya ya ubavu wa kushoto hasa wakati wa kulala huisha yenyewe kulingana na chanzo chake,ila kuna wakati linakuwa ni tatizo la muda mrefu ambalo huhitaji Tiba kamili,katika makala hii tumechambua kuhusu vyanzo mbali mbali vya tatizo hili pamoja na Tiba yake.

CHANZO CHA TATIZO LA KUUMWA UBAVU WA KUSHOTO WAKATI WA KULALA

kuna sababu mbali mbali ambazo huweza kupelekea mtu kupatwa na tatizo hili la maumivu makali ya ubavu wa kushoto wakati wa kulala na sababu hizo ni kama vile;

1. Tatizo la kuvimba,kuharibiwa au kupasuka kwa bandama au wengu huweza kusababisha matatizo mbali mbali kwa mgonjwa ikiwemo; kupata maumivu makali ubavu wa kushoto,kupata kizunguzungu,kutokuona vizuri,mgonjwa kuchoka sana,kichefuchefu n.k

Kuvimba kwa bandama au wengu huweza kuchangiwa na sababu mbali mbali kama vile; maambukizi ya virusi kama mononucleosis,maambukizi ya bacteria kama kaswende(syphilis), maambukizi ya parasite kama Malaria,magonjwa ya ini,damu n.k

2. Kupatwa na tatizo la kuvunjika kwa mbavu au kupata majeraha kwenye mbavu kutokana na sababu mbali mbali kama vile ajali,kuanguka n.k

3. Tatizo la Costochondritis, hili ni tatizo ambalo huhusisha kuvimba kwa gegedu yaani Cartilage ambazo zimejishikiza kwenye mbavu hasa upande wa kushoto,kuvimba kwa cartilage hizo hutokana na sababu mbali mbali ikiwemo; maambukizi ya vimelea vya magonjwa,kuumia,tatizo la arthritis n.k

4. Tatizo la kuvimba kwa kongosho yaani pancreatitis, Mtu mwenye shida hii huanza kupata maumivu taratibu ambayo huongezeka kadri siku zinavyokwenda hasa baada ya kula chakula, kuvimba kwa kongosho huweza kutokana na sababu kama vile; kuumia,matumzi ya pombe kupita kiasi,tatizo la gallstones n.k

5. Tatizo la kuvimba kwa kuta za tumbo yaani Gastritis, hasa kwenye eneo la upande wa kushoto karibu kabsa na mbavu zako,tatizo hili huweza kusababisha maumivu makali ya ubavu wa kushoto hasa wakati wa kulala,

Kuvimba kwa kuta za tumbo huweza kutokana na sababu mbali mbali kama vile; maambukizi ya bacteria au virusi,matumizi ya pombe kupita kiasi,matumizi ya dawa jamii ya nonsteroidal anti inflammatory(NSAIDs) kwa kiasi kikubwa n.k

6. Maambukizi kwenye figo au tatizo la mawe kwenye figo(kidney stones), watu wenye shida hii huweza kupata tatizo la maumivu ya ubavu wa kushoto pia

7. Kuvimba kwa pericardium kutokana na sababu mbali mbali kama vile maambukizi ya magonjwa,kuumia,matumizi ya dawa jamii ya anti-seizures kwa kiasi kikubwa n.k

8. Tatizo la kuvimba kwa tissue zinazofunika mapafu yaani Pleurisy, kutokana na sababu mbali mbali kama vile kuumia,maambukizi ya magonjwa, Bacteria,virusi,fungal pneumonia n.k

9.Lakini pia mtu huweza kupata maumivu ya ubavu wa kushoto baada ya kulala vibaya,japo maumivu haya hayawezi kudumu kwa muda mrefu sana.

DALILI ZA HATARI KWA MTU MWENYE MAUMIVU MAKALI YA UBAVU WA KUSHOTO

Muone daktari haraka Endapo unapata maumivu makali ya ubavu wa kushoto lakini yanaambatana na:

– Tatizo la kushindwa kupumua au kukosa pumzi

-Tatizo la kutokwa na jasho kupita kiasi

– Maumivu makali ya kichwa

– Kupatwa na kizunguzungu kikali

– Mtu kuonyesha dalili zote za kuchanganyikiwa n.k

VIPIMO

Mtu mwenye tatizo la maumivu ya ubavu wa kushoto huweza kupimwa kwa;

• kuangaliwa na kuminywa sehemu ya tatizo yaani physical examination

• Kipimo cha Electrocardiogram

• Vipimo vya damu pamoja na mkojo

• X-ray, CT scan au MRI

MATIBABU YA TATIZO LA KUUMWA UBAVU WA KUSHOTO WAKATI WA KULALA

Tiba ya tatizo hili hutegemea na chanzo husika,hivo kama chanzo ni kuvimba basi mgonjwa atapewa dawa jamii ya nonsteroidal anti inflammatory drugs(NSAIDs) kupunguza maumivu pamoja na uvimbe, kama tatizo ni maambukizi ya bacteria mgonjwa atapewa antibiotics mbali mbali n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.