Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

HATUA MUHIMU ZA KUZINGATIA UNAWAPO MIKONO

Katika swala la kunawa mikono,bado kuna msisitizo mkubwa kutoka kwa wataalam wa afya sio kwa sababu ya kukukinga tu na ugonjwa wa UVIKO-19 au COVID-19 bali tabia hii itakukinga na magonjwa mengine mengi kama vile; kuharisha(kipindupindu),homa ya matumbo n.k

Leo katika makala hii tunakumbushana kuhusu hatua muhimu za kuzingatia wakati wa unawaji mikono yako, yapo baadhi ya mambo muhimu sana ambayo unatakiwa kuyaangalia wakati unafanya zoezi hili la kunawa mikono yako.

Kwanza kabsa kabla ya kuangalia hatua hizo,hakikisha umeandaa mazingira yako ya kufanya zoezi hili la kunawa mikono yako,ikiwa ni pamoja na kuwa na Maji tiririka,Sabuni n.k

BAADHI YA HATUA ZA KUZINGATIA WAKATI WA KUNAWA MIKONO NI PAMOJA NA;

1. Loanisha mikono yako kwa maji tiririka kama kwenye picha hapo chini

2. Paka sabuni mikono yako miwili kama kwenye picha hapo chini.

3. Katika zoezi la kusugua mikono hakikisha unasugua mikono yako nje,ndani na sehemu zote za vificho kama kwenye picha hapo chini

4. Baada ya hapo hakikisha unakausha vizuri mikono yako,

Pia endelea kuchukua tahadhari zaidi dhidi ya Uviko 19, Fanya maamuzi ya kujikinga na kuwakinga uwapendao,KACHANJE sasa.

5.Kwa maelekezo zaidi Piga namba 199 bila Malipo, Via @Elimu_ya_afya

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.