Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Wiki ya Chanjo Duniani(24-30 April World Immunization week)

Wiki ya Chanjo Duniani(24-30 April World Immunization week)

Kila mwaka kuna Wiki ya Chanjo Duniani,jumuiya mbali mbali za kimataifa hukusanyika kusherehekea nguvu ya pamoja ya kuokoa maisha kwa kutumia chanjo.

Moja ya Lengo kubwa ni kuongeza ufahamu juu ya chanjo na Umuhimu wa kupata chanjo hasa kwa watoto waliokosa chanjo zinazosaidia kuwalinda dhidi ya magonjwa, ulemavu na hata Vifo.

Hakuna Mtoto Anayepaswa Kukosa Chanjo ambayo itamsaidia Kuokoa Uhai wake,
Katika kila eneo la dunia, milipuko ya magonjwa yanayoweza kuzuilika kama surua, polio, na dondakoo inaongezeka.

Mnamo 2021, watoto milioni 25 walikosa angalau chanjo moja ya zile chanjo za kawaida(routine vaccine) na milioni 18 hawakupokea chanjo ya aina yoyote.

Mnamo mwaka wa 2021, karibu watoto milioni 40 waliachwa katika hatari ya kushambuliwa na surua, na inakadiriwa 128,000 walikufa kwa surua.

Mnamo 2021 na 2022, milipuko ya polio iligunduliwa katika maeneo yenye viwango vya chini vya chanjo. Visa vya kupooza kutokana na polio vilipatikana pia hata maeneo kama Marekani na London.

Hakuna mtoto anayepaswa kunyimwa haki ya chanjo ya kuokoa maisha. Ni lazima tupate haraka na kuwachanja watoto ambao walikosa chanjo. CDC inaunga mkono”

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.