Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

UGONJWA WA MULTIPLE SCLEROSIS,CHANZO,DALILI NA TIBA YAKE

Mutiple Sclerosis ni ugonjwa ambao huhusisha hitilafu kwenye mfumo mkuu wa fahamu(central nervous system) nikiwa na maana ya ubongo pamoja na uti wa mgongo.

Kwenye tatizo hili  mfumo wa kinga ya mwili huweza kushambulia Protective Sheath au MYELIN ambayo hufunika Nerves fibers na kusababisha shida ya mawasiliano kati ya Ubongo pamoja na sehemu zingine za mwili,

Ukweli ni kwamba tatizo hili huweza kusababisha uharibifu wa kudumu wa Nerves kwenye mwili wako.

DALILI ZA TATIZO LA MULTIPLE SCLEROSIS NI PAMOJA NA;

– Mtu kushindwa kabsa kutembea au kupata shida wakati wa kutembea

– Mtu kupata tatizo la Mguu mmoja au yote miwili kufa ganzi/kuwa dhaifu

– Mtu kuhisi hali ya shot kwenye mwili wake

– Mtu kuwa na tatizo la Mwili kutetemeka wenyewe bila sababu inayoeleweka

– Mtu kutembea hatua za matege au unstable gait tatizo ambalo hakuwa nalo hapo kabla

– Mtu kupatwa na tatizo la macho kutokuona vizuri,tatizo la kuona marue rue n.k

– Mwili kuchoka kupita kiasi hata kama hujafanya kazi yoyote ngumu

– Mtu kupata shida ya kuongea au kuwa na tatizo la kigugumizi,shida ambayo hakuwa nayo hapo kabla

– Mtu kupatwa na tatizo la Kizunguzungu

– Mtu kupatwa na matatizo mbali mbali ya uzazi

– Mtu kupatwa na tatizo la kibofu cha mkojo kushindwa kufanya kazi vizuri n.k

CHANZO CHA TATIZO LA MUTIPLE SCLEROSIS

Mpaka sasa Chanzo kamili cha Ugonjwa huu hakijulikani, ila kuna baadhi ya sababu ambazo zinaweza kuongeza uwezekano wa mtu kupata shida hii, na sababu hizo nikama vile;

1. Umri; Tafiti zinaonyesha kwamba watu wenye umri kati ya miaka 20 mpaka 40 hupatwa zaidi na shida hii

2. Jinsia; ugonjwa huu huwapata zaidi Wanawake kuliko wanaume

3. Ugonjwa huu hutokea zaidi kwa watu ambao ndani ya Familia zao kuna shida hyo

4. Ugonjwa huu huweza kuwapata watu wenye maambukizi ya magonjwa mbali mbali kama vile; Virusi vya Epstein Barr n.k

5. Pia shida hii huwapata zaidi watu kutoka Northern Europe kuliko maeneo mengine kama Africa n.k

6. Pia hali ya hewa ya sehemu kama vile Temperate Climate huweza kuchangia uwepo wa tatizo hili

7. Vitamin D; Tafiti zinaonyesha kwamba kuwa na kiwango kidogo sana cha vitamin D pamoja na kutokupatwa na jua kwa muda mrefu huweza kuongeza uwezekano wa tatizo hili kutokea

8. Pia magonjwa ya mfumo wa kinga ya mwili yaani Autoimmune diseases ikiwemo pia magonjwa kama ya Tezi la Thyroid, Pernicious anemia,Psoriasis,type 1 Diabetes n.k

9. Watu wanaovuta sigara wapo pia kwenye hatari ya kupatwa na tatizo hili la Multiple Sclerosis kuliko wale ambao hawavuti sigara.

MATIBABU YA UGONJWA WA MULTIPLE SCLEROSIS

– Mpaka sasa hakuna tiba ya kutibu kabsa ugonjwa huu,ila kuna matibabu ya kudhibiti tu dalili mbali mbali ambazo huweza kusababishwa na tatizo hili.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE LILE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.