Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

CHANZO CHA TATIZO LA HIATUS HERNIA,DALILI NA MATIBABU YAKE

CHANZO CHA TATIZO LA HIATUS HERNIA,DALILI NA MATIBABU YAKE

Hiatus hernia ni aina ya hernia ambayo huhusisha tumbo la chakula(stomach) kuvimba kuelekea kwa juu ya kifua kutokana na uwazi unaotokea kwenye eneo la Diaphragm(misuli inayotenganisha sehemu hizi mbili, tumbo la chakula pamoja na kifua chako),

DALILI ZA TATIZO LA HIATUS HERNIA NI PAMOJA NA;

– Mtu kupatwa na shida ya kiungulia mara kwa mara,kutokana na hali ya content za tumboni kurudi juu yaani Gastroesophageal reflux disease(GERD)

– Mtu kupata maumivu kwenye eneo la kifuani

– Mtu kupatwa na shida ya tumbo kujaa gesi mara kwa mara

– Mtu kupata shida wakati wa kumeza kitu chochote ikiwemo chakula

– Mtu kupata kichefuchefu pamoja na kutapika

– Chakula au kinywaji chochote kurudi juu muda mfupi tu baada ya kula au kunywa

– Mtu kupata shida ya kukosa hewa au pumzi

– Mtu kukosa choo au wengine kujisaidia na kutoa gesi sana wakati wa kujisaidia

CHANZO CHA HIATUS HERNIA NI NINI?

Mpaka sasa hakuna sababu ya moja kwa moja ya kutokea kwa aina hii ya hernia,ila kuna baadhi ya sababu zimeonekana kuongeza uwezekano wa kutokea kwa tatizo hili na sababu hizo ni kama vile;

1. Mtu kuzaliwa na uwazi mkubwa kwenye eneo linalotenganisha tumbo la chakula na kifua chake

2. Mtu kupatwa na majeraha ya aina yoyote kwenye eneo linalotenganisha tumboni na kifuani

3. Mabadiliko makubwa kwenye misuli ya Diaphragm kadri umri unavyokuwa mkubwa zaidi

4. Kuwepo kwa mgandamizo(Pressure) mkubwa eneo la tumboni kutokana na sababu mbali mbali kama vile;

• Kutokana na kunyanyua vitu vizito sana kama wafanya mazoezi maarufu kama Jim

• Mgandamizo mkubwa tumboni wakati wa ujauzito

• Mgandamizo mkubwa tumboni kutokana na unene/uzito kupita kiasi au Obesity

• Mgandamizo mkubwa tumboni kutokana na kuvaa mkanda unaobana sana tumbo mara kwa mara au kuvaa nguo za kubana tumbo sana mara kwa mara

• Mgandamizo mkubwa tumboni kutokana na mtu kukohoa sana mara kwa mara

• Mgandamizo mkubwa tumboni kutokana na mtu kujikaza sana wakati wa kujisaidia chooni mara kwa mara n.k

MATIBABU YA TATIZO HILI LA HIATUS HERNIA

– Matibabu yapo ya aina mbali mbali ikiwemo; kudhibiti dalili za hiatus hernia kama vile mtu kupewa dawa jamii ya Antiacids kutokana na kupata kiungulia mara kwa mara,

Matumizi ya Prokinetics kwa ajili ya kufanya misuli ya Esophageal sphincter kuwa imara zaidi,

Huduma ya upasuaji hasa kwenye aina hii ya paraesophageal hernia n.k

VITU VYA KUEPUKA AU VITU VYA KUFANYA UKIWA NYUMBANI KAMA UNA SHIDA HII YA HIATUS HERNIA,

✓ Usifanye mazoezi ya mwili au kuinamisha kichwa chini muda mfupi tu baada ya kula mfano ndani ya masaa 3 au 4

✓ Epuka kula vyakula vyenye acids sana kama vile; tomatosauce,maharage n.k

✓ Epuka kula vyakula venye viungo vingi sana au pilipili

✓ Epuka kula vyakula vyenye mafuta mengi sana

✓ Usile chakula kingi sana kwa wakati mmoja,Kula kidogo kidogo na taratibu;mfano unaweza kula milo midogo midogo 4 mpaka 5 kwa siku

✓ Epuka kunyanyua vitu vizito sana

✓ Epuka kuvaa nguo za kubana sana tumbo lako, kuvaa mikanda tumboni n.k

✓ Epuka kuvaa viatu vyenye visigino virefu sana

✓ Nyanyua kichwa chako angalau Nchi 6 wakati upo kitandani

✓ Epuka uvutaji wa sigara na unywaji wa Pombe

✓ Hakikisha unapunguza uzito wa mwili kama unauzito uliopitiliza n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

 

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.