Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

JE KWANINI NI MUHIMU KUZINGATIA ULAJI MZURI?

ULAJI

• • • • • •

JE KWANINI NI MUHIMU KUZINGATIA ULAJI MZURI?


Ulaji unaofaa ni pamoja na kula chakula mchanganyiko, cha kutosha na chenye virutubishi vyote kwa uwiano unaotakiwa. Kula matunda angalau mara mbili kwa siku na kula mboga mboga kwa wingi.

Ulaji unaofaa ni lazima uzingatie matumizi ya mafuta kwa kiasi kidogo. Mafuta ya nyama sio mazuri sana kwani yanahusishwa na magonjwa ya moyo, badala yake inashauriwa kutumia zaidi mafuta yatokanayo na mimea. 

Kama vile mafuta ya alizeti n.k

Matumizi ya sukari na chumvi yawe ya kiasi. Pia kwa watu wanaokunywa pombe wasinywe kupita kiasi.


KULA CHAKULA MCHANGANYIKO

Chakula mchanganyiko hukuwezesha kupata virutubishi vyote vinavyohitajika mwilini, kwa mfano vyakula vya wanga vinasaidia kuupa mwili nguvu na joto, utomwili husaidia kujenga mwili, vitamini na madini hulinda mwili dhidi ya magonjwa. Kila siku jitahidi kula vyakula kutoka katika makundi yafuatatyo:  Vyakula vya asili ya nafaka, ndizi za kupika na mizizi

 Vyakula vya jamii ya kunde, asili ya wanyama na mbegu za mafuta

 Mboga mboga

 Matunda

 Sukari, asali na mafuta


KUTOKULA MAFUTA MENGI

Mafuta mengi mwilini hasa yale yenye asili ya wanyama yanaweza kusababisha ongezeko la magonjwa ya moyo na shinikizo kubwa la damu, hivyo inashauriwa kutumia zaidi mafuta yatokanayo na mimea.  JINSI YA KUPUNGUZA MAFUTA:

 Tumia mafuta kidogo wakati wa kupika

 Epuka kula vyakula vilivyokaangwa kwa mafuta badala yake chemsha, oka au choma

 Punguza mafuta kwenye nyama iliyonona, na ikibidi ondoa ngozi ya kuku kabla ya kupika.

 Chagua nyama au samaki wasio na mafuta mengi.

Kula matunda na mbogamboga kwa wingi

Vyakula hivi huupatia mwili kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali kama vile baadhi ya magonjwa ya moyo, saratani na kisukari.


MATUNDA NI CHANZO CHA VIRUTUBISHO/VIINILISHE VYA VITAMINI NA MADINI 

ambavyo hupatikana kwa wingi kwenye vyakula hivi kuliko kwenye vyakula vingine. Virutubisho hivi:  huifanya ngozi kuwa ng’aavu na yenye afya na vidonda kupona vizuri

 huwezesha macho kuona vizuri

 husaidia kuimarisha ufahamu

 husaidia uyeyushaji wa vyakula tumboni na kufyonza madini mwilini

 hutumika katika kutengeneza damu

 husaidia katika uundaji wa chembe za uzazi.



Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.