Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

JINSI YA KUTATUA TATIZO LA KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA KWA WANAUME

JINSI YA KUTATUA TATIZO LA KUKOSA HAMU YA TENDO LA NDOA KWA WANAUME

Mambo ya kufanya ili kuongeza hamu ya tendo la ndoa yapo mengi. Hapa yapo machache ninayoweza kukushauri ili ujue jinsi unavyotakiwa kufanya ili kuongeza hamu ya tendo la ndoa.

Mambo hayo ni kama yafuatayo;

– MAZOEZI- Kukosa hamu ya tendo la ndoa ni kwa sababu viungo fulani vimetulia pasipo kufanya kazi.

Mazoezi huongeza ufanisi wa mzunguko wa damu,jambo linaloleta ufanisi wa tendo la ndoa.

Kama umekuwa unafanya mazoezi,hebu ongeza tena kiasi fulani na kuongeza hamu na ufanisi katika ufanyaji wa tendo la ndoa.

– MRIDHISHE Mke wako- Kukosa hamu ya tendo la ndoa pengine huwa ni matokeo ya tendo lililopita.

Si mara zote tendo la ndoa hufanyika kwa ufanisi. Takribani 40% hadi 50% tu ya matendo ya ndoa huwa katika uthabiti na wote kufurahia.

Kama mwanzoni hukumridhisha Mke wako, atatarajia awamu nyingine wewe kufanya vyema zaidi kuliko hapo mwanzo.

Jitahidi kuondoa hofu na wasiwasi huku ukijiamini ili umridhishe Mke wako na ukidhi matamanio yake.

– JADILIANENI Pamoja- Kujadiliana kwa pamoja hukusaidia kumfanyia Mke wako kile anachokitaka na yeye kukufanyia kile unachotaka.

Hii itaongeza hamu yako kwa kuwa utapata unachotaka na Mke wako pia atapata anachotaka.

– JENGA MATAMANIO kwa Mke wako- Tendo la ndoa huazia akilini. Jenga mazoea ya kumwona Mke wako kama bora sana na kitu atakachokufanyia ni bora sana pia.

Unapopanga kushiriki kufanya tendo na Mke wako,jenga picha akilini ya matamanio kwake na hii itakusaidia kuepuka kukosa hamu ya kushiriki na Mke wako.

– TUMIA CHAKULA bora- Kuna uwezekano wa kutumia chakula ili kuongeza hamu ya kufanya tendo la ndoa.

Mchanganyiko wa chakula cha WANGA kwa asilimia 40-50 , PROTEIN 25% -35%, FATS kwa 25%-30% na MATUNDA kwa wingi kama vile TIKITI MAJI,husaidia kuongeza hamu ya kufanya tendo la ndoa.

Pia virutubisho kama ZINC huweza kukusaidia pia kuongeza uwezo na hamu ya kufanya tendo la ndoa.

– EPUKA msongo wa mawazo- Kama tulivyoona hapo juu,msongo wa mawazo huweza kusababisha kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa, kuepuka msongo kutakusaidia kufanya tendo la ndoa kwa ufanisi.

– MFUMO wa maisha- Kama unataka kuepuka tatizo la kukosa hamu ya kufanya tendo la ndoa, ACHA pombe , ACHA pia kutumia madawa ya kulevya kama vile marijuana , Mirungi na mengineyo.

– Kama bado tatizo lipo kutana na wataalam wa afya kwa ajili ya kuanza tiba kamili ya tatizo hili

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO HILI TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.