Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

UMUHIMU WA KUNAWA MIKONO(jikinge na magonjwa)

UMUHIMU WA KUNAWA MIKONO(jikinge na magonjwa)

Moja ya hatua muhimu kwenye afya ambayo huweza kutusaidia sisi kujikinga na magonjwa pamoja na kuzuia kuwasambazia wengine ni pamoja na hii ya Kunawa mikono na Sabuni kila mara.

Japo watu wengi huona hili ni jambo la kawaida sana ambalo sio la kuzingatia sana,ila fahamu magonjwa mengi pamoja na vimelea vya magonjwa huwashambulia watu kwa kutokunawa mikono na maji safi,yenye kutiririka pamoja na Sabuni.

NI KIVIPI VIMELEA HAWA WA MAGONJWA HUWASHAMBULIA WATU KISHA KUSABABISHA WATU KUUMWA?

Kinyesi cha binadamu pamoja na Wanyama mbali mbali ni chanzo kikubwa sana cha vimelea vya magonjwa(germs) kama vile; Salmonella, E. coli au norovirus,

ambao huweza kusababisha mtu kupata tatizo la kuharisha,kipindu pindu,homa ya matumbo(typhoid), magonjwa ya ngozi, magonjwa ya macho na wengine kuathiri mpaka mfumo wa upumuaji(respiratory infections) kama vile adenovirus,Corona Virus n.k

VIMELEA(germs) wote hawa huweza kuwapata watu kupitia kwenye mikono,baada ya watu kwenda chooni au kubadilisha diaper bila kunawa mikono vizuri, na wakati mwingine hata ukiwa unakata nyama za mbuzi,ng’ombe n.k ili upike,au kushika kitu chochote kichafu chenye vimelea hawa,kushikana mikono na watu,kugusana n.k,

unaweza kushika vinyesi hivi vya wanyama,watu au kushika kitu chochote kichafu chenye vimelea hawa na kupata wadudu hawa,usiponawa mikono vizuri unaweza kuwapeleka mdomoni kisha mwilini.

FAHAMU: Gram moja ya kinyesi cha binadamu inaweza kuwa na takribani vimelea(germs) trillion moja

Hivo basi,Kunawa mikono na maji safi,yenye kutiririka pamoja na Sabuni husaidia sana kuwaondoa hawa vimelea baada ya kuwapata kwa kushika vitu vyenye vimelea hawa.

Nawa mikono vizuri baada ya kutoka toilet,kushika nyama wakati unazikata ili upike, baada ya kutoka kwenye mihangaiko yako ya maisha,kabla ya kula na kunywa kitu chochote.

KUMBUKA:Kunawa mikono na maji safi,yenye kutiririka pamoja na Sabuni ni kinga tosha dhidi ya magonjwa mbali mbali.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.