Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Abiria anasa chooni safari yote ya ndege angani

Abiria anasa chooni safari yote ya ndege angani

India. Abiria amekwama ndani ya choo cha ndege kwa muda wa dakika 105 za safari yote ya ndege, muda mfupi baada ya kuruka kwenye uwanja wa ndege wa Mumbai.

Kwa mujibu wa gazeti la The Times of India, tukio lilitokea Jumatatu Januari 15, 2024 wakati ndege ya kampuni ya SpiceJet ilipoondoka kwenye uwanja wa ndege wa Mumbai saa 10.55 jioni kwenda katika mji wa Bengaluru ambako ni mwendo wa dakika 105  angani.

Kwa mujibu wa taarifa za maofisa wa kampuni hiyo, abiria huyo baada ya ndege kuruka alikwenda kujisaidia, lakini mlango ulijifunga na kushindwa kutoka kwa muda wote wa safari hadi ilipotua katika Jiji la Bengaluru.

Taarifa zilisema kitasa cha mlango wa choo kiliharibika na hivyo kuwa ngumu kuufungua kwa ndani na nje.

“Lakini, abiria alipojaribu kufungua mlango wa choo kidogo, aligundua kwamba hangeweza kutoka baada ya kitasa kuharibika,” ilisema taarifa ya kampuni hiyo.

Taarifa ilisema abiria huyo alipiga kelele kuomba msaada na wafanyakazi wa ndani ya ndege waliokwenda kutoa msaada, nao hawakuweza kuufungua mlango huo.

Taarifa ilisema abiria huyo aliokolewa na mafundi baada ya ndege kutua Bengaluru saa 3.42 asubuhi Jumanne.

Kwa mujibu wa taarifa, mafundi baada ya kuufungua mlango wa choo walimkuta abiria huyo akiwa katika hali ya mshtuko na baada ya kutoka alipewa huduma ya kwanza na madaktari uwanjani hapo.

“Ilijulikana kuwa abiria aliyekuwa kwenye kiti namba 14D alikuwa ameenda chooni mara tu baada ya ndege kupaa na alama za mikanda ya usalama kuzimwa.

“Cha kusikitisha alinasa ndani baada ya kitasa cha mlango wa choo kuharibika,” alisema ofisa ambaye hakutaja jina katika uwanja wa ndege wa Bengaluru.

Ofisa huyo alisema wafanyakazi wa ndani ya ndege walijaribu kufungua mlango uliokuwa umekwama baada ya kusikia kilio cha mwanamume huyo bila mafanikio.

Alisema muda mfupi kabla ya ndege kutua, mhudumu wa ndege aliingiza chooni kupitia chini ya mlango kikaratasi chenye maandishi ya kumtaka abiria huyo asiwe na hofu na ajiandae kutua kwenye uwanja wa ndege wa Bengaluru.

Ujumbe ulisomeka: ‘Bwana, tulijaribu tuwezavyo kuufungua mlango… Usiogope. Tunatua baada ya dakika chache, kwa hivyo tafadhali funga kifuniko cha choo na ukae juu yake na ujilinde. Mara tu mlango mkuu utakapofunguliwa, mhandisi atakuja.’

Taarifa kampuni ya SpiceJet ya kuomba radhi ilisema inajutia usumbufu uliompata abiria huyo na kuongeza kuwa amerudishiwa nauli yake kamili.

“Katika safari nzima, wafanyakazi wetu walitoa usaidizi na mwongozo kwa abiria. Baada ya kuwasili, mhandisi alifungua mlango wa choo na abiria akapata usaidizi wa haraka wa matibabu,”  ilisema taarifa ya kampuni hiyo.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.