Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

MATUMIZI YA PARACETAMOL PAMOJA NA TAHADHARI ZAKE

MATUMIZI YA PARACETAMOL PAMOJA NA TAHADHARI ZAKE

Ni dhahiri kwamba dawa ya Paracetamol au paracetum ni dawa ambayo hutumika sana kwenye maisha yetu ya kila siku, na pengine kwa umaarufu wake, wengine wamekuwa wakiitumia hata kwenye matibabu ambayo hayahitaji dawa hii.

Je wajua dawa ya Paracetum hutibu kitu gani? endelea kufwatilia makala hii uweze kujua kuhusu matumizi ya dawa hii ya paracetum pamoja na tahadhari zake.

MATUMIZI YA PARACETAMOL:

Dawa ya paracetum hutumika kutibu matatizo mbali mbali kama vile;

– Maumivu madogo(mild) au maumivu ambayo yapo kwenye level ya wastani yaani moderate,

Hapa nazungumzia maumivu ya aina mbali mbali kama vile;

1. Maumivu ya kichwa yaani headaches

2. Maumivu ya jino yaani toothaches

3. Maumivu wakati wa hedhi au menstrual period kwa wanawake

4. Maumivu ya mgongo yaani backaches N.K

– Pia paracetum huweza kutumika kwa mtu mwenye Tatizo la osteoarthritis

– Paracetum ni dawa nzuri sana kwa ajili ya kushusha homa(reduce fever).

TAHADHARI KWENYE MATUMIZI YA DAWA HII YA PARACETAMOL(Warnings)

• Matumizi ya kiwango kikubwa cha dawa hii ya paracetamol huweza kusababisha shida kubwa ya Ini;serious (possibly fatal) liver disease.

Hivo epuka kutumia dawa hizi hovio pasipo maelekezo kutoka kwa wataalam wa afya

• Watu wenye matatizo ya Ini pamoja na Watoto wanashauriwa kutumia kiwango kidogo sana cha dawa hii

• Usitumie dawa hii pamoja na dawa zingine zenye acetaminophen bila kupewa maelekezo ya wataalam wa afya

• Pata msaada wa haraka kutoka kwa wataalam wa afya kama umeoverdose dawa hizi au umeanza kupata dalili kama hizi baada ya kutumia dawa;

– Kichefuchefu pamoja na kutapika sana

– Kukosa kabsa hamu ya kula chakula

– Kutoa jasho sana

– Maumivu makali ya tumbo

– Uchovu wa mwili kupita kiasi ambao haukuwa nao hapo kabla

– Macho na ngozi kuanza kubadilika rangi na kuwa yamanjano

– Kukojoa mkojo mweusi N.k

• Epuka Matumizi ya dawa hizi za paracetum(acetaminophen) pamoja na Pombe kila siku kwani huweza kuharibu kabsa Ini lako.

• Kama unampa mtoto dawa hii hakikisha sana unampa dose ambayo hutakiwa kwa watoto pamoja na aina za paracetum mahususi kwa watoto kama vile aina za syrup n.k

• Na kama dawa hii ipo mfumo wa suspensions, hakikisha unashake vizuri kabla ya kumpa

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.