Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Tatizo la Mtu kuwa na sehemu za Siri Mbili(hermaphroditism)

Tatizo la Mtu kuwa na sehemu za Siri Mbili(hermaphroditism),Dalili,Chanzo,Tiba

Tatizo hili huhusisha Mtoto kuzaliwa akiwa na Mifumo ya Jinsia mbili yaani male and female reproductive organs,

Hivo mtoto huyu anakuwa na vyia vya uzazi vya Mwanaume, na via vya uzazi Jinsia ya Kike.

Tatizo hili kwa Kitaalam hujulikana kama hermaphroditism

DALILI ZA TATIZO HILI LA HERMAPHRODITISM NI PAMOJA NA;

Kulingana na hali ilivyo,hizi hapa ni baadhi ya dalili na Ishara mbali mbali za Hali hii kwa Mtu;

– Kuwa na Sehemu za Siri zenye utata, yaani unashindwa kuelewa huyu ni Mwanaume au Mwanamke(Ambiguous genitalia)

– Kuwa na Uume mdogo sana sana

– Kuwa na Kinembe kikubwa kuliko kawaida(Clitoromegaly)

– Korodani kutokushuka chini kama kawaida

– Sehemu ya mashavu ya Uke kuungana(Labial fusion)

– Kuchelewa sana kufikia balehe,au kutokuwa na mabadiliko yoyote ya mwili ambayo ni yakiukuaji kama mtu mzima,

hapa nazungumzia mabadiliko ambayo tunategemea yatokee kipindi cha ukuaji yani kipindi cha balehe

– Kuwa na tatizo la tundu chini ya Uume,ambapo kitaalam hujulikana kama Hypospadias,

Hii hupelekea hata mtoto akikojoa mkojo badala kutokea mbele kwenye tundu kama kawaida,hutokea kwa chini ya uume.

JINSI YA KUTAMBUA TATIZO HILI LA HERMAPHRODITISM

Vipimo mbali mbali huweza kufanyika ikiwemo;

• Kipimo cha Uchambuzi wa Chromosomes(yaani Chromosomes analysis)

•Vipimo vya damu(Blood tests), kwa ajili ya kuchunguza kiwango cha Hormones Pamoja na Kiwango cha Electrolytes

• Kipimo cha Endoscopic,

• Kipimo cha Molecular testing

• Kipimo cha Ultrasound, MRI, N.k

MATIBABU YA TATIZO HILI LA HERMAPHRODITISM

Mtoto mwenye tatizo hili atahitaji uchunguzi wa Kina na matibabu kutokwa kwa Jopo la Wataalam wa Afya,

Tiba inaweza kuhusisha UPASUAJI, Matibabu kwenye hormones yaani Hormonal therapy n.k

Hapa Kuna Mjadala Mkubwa Duniani kwenye Maswala ya Kiubaguzi(Stigma) kuhusu Jinsia ya Mtoto, Kwani Hapo Awali Mtoto alikuwa anaelekezwa kwenye jinsia Moja mapema mno kwa kuangalia Via vya Uzazi vya Nje,

Ila kutokana na maendeleo ya Sayansi na Technolojia vyote vinawezekana,

SWALI LINAKUJA; Je Tumfanye awe na Jinsia ya KIKE au YAKIUME?

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.