Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

TATIZO LA KUTAFUNA NYAMA ZA PEMBENI YA LIPS

TATIZO LA KUTAFUNA NYAMA ZA PEMBENI YA LIPS

Baadhi ya watu wana tabia ya kung’ata na kutoa nyama za kwenye Lips, na baadhi yao hufanya sana hasa wakiwa kwenye hali ya wasi wasi, ila wengine ni tabia ambao wameizoea kila siku.

Wakati mwingine hadi husababisha michubuko,vidonda, na wekundu sana kwenye lips za mdomo.

CHANZO CHA HALI HII NI NINI?

– Unaweza kujing’ata kwenye lips au kutafuna nyama za pembeni ya lips kwa bahati mbaya wakati unaongea au wakati unatafuna kitu kama chakula n.k

– Ila kwa baadhi ya watu ni hali ambayo hutokea wakiwa kwenye wasiwasi mkubwa,hofu au Msongo wa mawazo(Stress),

– kuconcentrate sana kwenye jambo flani

– Hali ya upweke sana

– Sababu zingine ni pamoja na;

• Tatizo la Teeth alignment ambalo kwa kitaalam hujulikana kama malocclusion.

• Tatizo la Temporomandibular disorder(TMD), ambapo tatizo hili huathiri misuli kwa ajili ya kutafuna yaani chewing muscles.

Watu wenye matatizo haya; malocclusion au TMD huweza kupatwa na hali ya kula au kutafuna lips za mdomo,ulimi n.k

• Lakini wakati mwingine huweza kuwa matatizo ya kisaikolojia, afya ya akili n.k, Mfano; tatizo hili likiwa ni Chronic lip biting huweza kuwa kiashiria cha body-focused repetitive behavior, or BFRB. N.k

na hapa huweza kuhusisha tabia mbali mbali kama vile; Mtu kuvuta nywele zake, Kula kucha, kung’ata Lips za mdomo, skin-picking au excoriation n.k

DALILI ZA MTU AMBAYE ANANG’ATA LIPS ZAKE,

Sio lazima dalili kuonekana,ila kwa baadhi huweza kuonyesha;

• Wekundu sana kupita kiasi kwenye Lips za mdomo

• Vidonda au michubuko kwenye Lips za mdomo

• Kuvimba kwa Lips N.k

MATIBABU YA TATIZO HILI

Jinsi ya kuacha pamoja na Tiba yake hutegemea chanzo chake, Hivo baada ya kugundua chanzo utapata Msaada wa haraka zaidi.

KWA USHAURI ZAIDI, MAWASILIANO NI +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.