Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Ganzi nyayoni inasababishwa na nini? Na nini tiba yake?

Ganzi nyayoni inasababishwa na nini? Na nini tiba yake?

Tatizo la kupata ganzi kwenye Nyayo au miguu kufa ganzi huweza kutokea kwa mtu yoyote,na tatizo hili huhusisha vyanzo zaidi ya kimoja,hivo uchunguzi wa kina unahitajika kufahamu chanzo cha tatizo lako,

Unaweza kupata Ganzi nyayoni au Miguu huweza kufa ganzi kwa muda mfupi lakini pia kwa baadhi ya watu hili ni tatizo la muda mrefu ambalo hujirudia mara kwa mara au la kudumu. je chanzo cha tatizo hili la miguu kufa ganzi ni nini? soma hapa katika makala hii

CHANZO CHA TATIZO LA MIGUU KUFA GANZI NI PAMOJA NA;

1. Mtu kukaa sehemu moja kwa muda mrefu, kukaa sehemu moja kwa muda mrefu huweza kuleta tatizo la miguu kufa ganzi japo ni kwa muda mfupi tu na kisha tatizo hili huisha lenyewe

2. Kukunja miguu kwa muda mrefu, mtu huweza kupata shida ya miguu kufa ganzi baada ya kuikunja kwa muda mrefu, japo tatizo hili pia sio la kudumu,huisha ndani ya muda mfupi hasa baada ya mtu kufanya mazoezi au kuanza kutembea, Kukunja miguu kwa muda mrefu huweza kusababisha pressure au mgandamizo ambao husababisha Nerves za miguuni kukosa mawasiliano mazuri na ubongo wako hivo kuleta tatizo la ganzi miguuni

Hali hii kwa kitaalam hujulikana kama PARESTHESIA, ambapo pia huweza kuambatana na matatizo mengine kama vile mtu kuhisi kuungua moto miguuni n.k

3. Sciatic Nerves ambayo hutoka sehemu ya chini mgongoni kupitia kwenye hips pamoja na matakoni kubanwa, hii huweza kusababisha tatizo la miguu kufa ganzi, Baada ya nerve hii ya SCIATIC kubanwa mtu huweza kupatwa na matatizo kama vile; miguu kufa ganzi, maumivu ya mgongo kushuka chini miguuni, maumivu ambayo huwa makali zaidi mtu akikohoa,kupiga chafya, au kukaa kwa muda sehemu moja,misuli ya miguuni kukosa nguvu n.k.

4. Ugonjwa wa KISUKARI, ugonjwa huu huweza kusababisha tatizo la uharibifu wa nerves hali ambayo hupelekea tatizo la ganzi,ndyo maana wagonjwa wengi wa kisukari hupata tatizo la miguu kufa ganzi pamoja na viungo vingine vya mwili kama vile mikono na vidole vyake n.k

Hali hii kwa kitaalam hujulikana kama PERIPHERAL NEUROPATHY ambapo nerves za maeneo kama vile ya miguuni,mikononi,kwenye vidole n.k huharibika, na hapa ndipo mgonjwa huanza kupata maumivu makali ya miguu na mikono hasa wakati wa usiku, misuli kukosa nguvu na kuwa dhaifu, Kupatwa na vidonda kwenye miguu,kupata maumivu makali ya miguu wakati ikiguswa n.k

5. Tatizo la Multiple Sclerosis, ambapo Kinga yako ya mwili ambayo inapambana na vimelea vya magonjwa mbali mbali huanza kushambulia mfumo wako mkuu wa fahamu yaani Central nerves system, kisha kusababisha matatizo kama vile; miguu kufa ganzi, kuhisi miguu kuchoma choma kama mtu anakuchoma na sindano, uchovu wa mwili kupita kiasi hata kama hujafanya kazi yoyote ngumu, misuli ya mwili kuwa dhaifu,kukakamaa mara kwa mara yaani muscle spasms,mtu kupata kizunguzungu, Kupatwa na matatizo ya macho kutokuona vizuri n.k

6. Matumizi ya pombe kupita kiasi,tafiti zinaonyesha kwamba, sumu inayotokana na matumizi ya pombe huweza kuharibu mfumo wa fahamu(Nerves) kisha kusababisha matatizo mbali mbali ikiwemo hili la miguu kufa ganzi

7.Kuwa na uvimbe au Peripheral nerves tumor, kukuwa kwa uvimbe kwenye eneo la Nerves za maeneo kama vile miguuni na mikononi huweza kusababisha tatizo la Nerves hizi kushindwa kudhibiti utendaji kazi wa misuli ya miguuni,kisha kuleta tatizo la miguu kufa ganzi,miguu kuvimba,misuli ya miguuni kuwa dhaifu au kukosa nguvu n.k

MATATIBABU YA TATIZO HILI LA MIGUU KUFA GANZI

– Zipo tiba za aina mbali mbali kulingana na chanzo husika, hivo mtu mwenye tatizo hili huweza kushauriwa kufanya vitu mbali mbali ikiwa ni pamoja na;

• Kufanya mazoezi ya mwili lakini pia mazoezi ambayo kwa kiasi kikubwa hugusa eneo la mikono pamoja na miguu yake

• Kuepuka kukaa sana sehemu moja kwa muda mrefu

• Kufanya massage ya miguuni,kula mlo kamili,kupata muda mzuri wa kulala

• Pamoja na matumizi ya dawa mbali mbali baada ya chanzo cha tatizo lake kugundulika, hivo wataalam wa afya huweza kushauri matumizi ya dawa mbali mbali kama vile; Dawa jamii ya Antidepressants kama Duloxetine, Dawa jamii ya Corticosteroids,N.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.