Je ni Muda gani wa kuanza dawa za ARVS baada ya kugundulika una HIV?
Je ni Muda gani wa kuanza dawa za ARVS baada ya kugundulika una HIV?
Zipo Dhana mbali mbali kwenye jamii kuhusu Muda wa Kuanza dawa za ARV baada ya kugundulika una Virusi vya UKIMWI,
Huku baadhi ya watu wakisema,hutakiwi kuanza dawa za ARV mpaka uanze kuumwa, je ni kweli?
Soma zaidi hapa chini…!!!
Tiba ya VVU inahusisha unywaji wa dawa zenye ufanisi mkubwa ziitwazo antiretroviral therapy (ART) ambazo hufanya kazi kudhibiti virusi.
ART inapendekezwa kwa kila mtu mwenye VVU.
Watu walio na VVU wanapaswa kuanza ART haraka iwezekanavyo baada ya utambuzi (hata siku hiyo hiyo).
Nimatumaini yangu kwamba umepata majibu kuhusu Muda wa kuanza dawa za kufubaza Virusi vya Ukimwi maarufu kama ARVs.