Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Watu ambao wapo kwenye hatari zaidi ya kupata Magonjwa ya Zinaa(STD’s)

Watu ambao wapo kwenye hatari zaidi ya kupata Magonjwa ya Zinaa(STD’s)

• • • • • •

KUNDI LA WATU AMBALO LIPO KWENYE HATARI YA KUPATA MAGONJWA YA ZINAA

Magonjwa ya zinaa ni magonjwa ambayo huweza kuambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kwa njia ya kujamiiana au kufanya ngono.

Magonjwa hayo ni pamoja na; Ugonjwa wa Kisonono, ugonjwa wa kaswende, Ugonjwa wa Chlamydia, Ugonjwa wa ukimwi N.k

MAGONJWA YA ZINAA AU KWA KITAALAM SEXUAL TRANSMITTED DISEASES-STD’s

haya ni magonjwa ambayo huenezwa kwa njia ya kufanya mapenzi, na magonjwa haya hutokana na mashambulizi ya vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile BACTERIA, VIRUSI,PARASITES n.k

HII HAPA CHINI NI ORODHA YA BAADHI YA MAGONJWA YA ZINAA(STD’s)

1. Ugonjwa wa Masundosundo yaani Genital Warts ambao husababishwa na kirusi aitwaye HUMAN PAPILLOMA VIRUS(HPV)

2. Tatizo la Genital Herpes/Genital shingles au kwa jina lingine Herpes Simplex

3. Ugonjwa wa Chlamydia

4. Ugonjwa wa Kaswende au Kwa kitaalam hujulikana kama Syphilis

5. Ugonjwa wa Kisonono maarufu kama Gono au Gonorrhea

6. Maambukizi ya Ukimwi HIV/AIDS

7. Tatizo la Trichomoniasis

8. Tatizo la Bacterial Vaginosis

9. Tatizo la Hepatitis N.K

KUNDI LA WATU AMBALO LIPO KWENYE HATARI YA KUPATA MAGONJWA YA ZINAA NI PAMOJA NA;

– Wanaofanya ngono zembe, yaani wanaofanya mapenzi bila kutumia kinga kama condom za kike au za kiume

– Wanaojishirikisha na kufanya mapenzi kinyume na maumbile

– Wale ambao wana wapenzi wengi au kwa kitaalam tunasema multiple sexual partners

– Wanywaji wa pombe au walevi

– Watumiaji wa madawa mengine ya kulevya ikiwa ni pamoja na sindano za kujidunga

– Wavutaji wa sigara

– Wajawazito kutokana na kushuka kwa kinga ya mwili kipindi cha ujauzito,hivo mwili kushindwa kupambana na magonjwa, na magonjwa kuingia na kushambulia mwili kwa urahisi zaidi.

N.K

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.