Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Chanzo cha Maumivu ya Shingo pamoja na Tiba yake

Chanzo cha Maumivu ya Shingo pamoja na Tiba yake

Moja ya vitu vinavyosababisha Maumivu ya shingo ni pamoja na tatizo la arthritis,  disc kuzorota na kuharibika, mfereji wa mgongo kuwa mwembamba sana, kuvimba kwa misuli, mkazo au Kuumia n.k.

Baadhi ya watu husumbuliwa sana na tatizo hili la maumivu makali ya shingo,na hizi ni baadhi ya sababu za tatizo hili

Baadhi ya Sababu za maumivu ya shingo ni pamoja na:

– Matatizo ya misuli kama Vile Misuli Kukaza. Matumizi ya misuli hii ya shingoni kupita kiasi,

kama vile kutumia muda mwingi sana ukiwa umeshikilia na kuinamia kompyuta au simu mara nyingi husababisha mkazo wa misuli.

Hata vitu vidogo, kama vile kusoma kitandani, vinaweza kukaza misuli ya shingo,

Lakini pia kulala vibaya wakati wa usku inaweza kupelekea kupata maumivu ya shingo yako.

– Matatizo kwenye Joints za shingoni yaani Neck joints.

Kama ilivyo kwenye joints zingine katika mwili, Joints za shingoni(neck joints) huweza kuzeeka, kupungua utendaji kazi wake pamoja na kuharibika kadri umri unavyokuwa mkubwa zaidi,

Kwa kukabiliana na uchakavu huu, mwili mara nyingi huunda spurs ya mfupa ambayo inaweza kuathiri mwendo yaani joints motion pamoja na kusababisha maumivu shingoni.

– Ukandamizaji wa neva yaani Nerve compression.

Tatizo la Herniated disks au kutokea kwa bone spurs kwenye pingili za shingoni huweza kusababisha mgandamizo wa Neva zinazotokea kwenye eneo la uti wa mgongo.

Hali hii huweza kupelekea mtu kupata maumivu ya shingo

– Majeraha au Kuumia, Pia mtu huweza kupata maumivu ya shingo baada ya kudondoka,kugongwa na kitu shingoni,au kupata ajali ya aina yoyote,

ambayo hupelekea kuumia,majeraha au kupata tatizo lolote eneo hili la shingoni.

– Magonjwa. Magonjwa mbali mbali kama vile rheumatoid arthritis, meningitis au saratani, yanaweza kusababisha maumivu ya shingo. n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.