Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Je kuna uhusiano gani kati ya hofu au Wasiwasi na mtu kupata mvurugiko wa tumbo pamoja na Kuharisha?

Je kuna uhusiano gani kati ya hofu au Wasiwasi na mtu kupata mvurugiko wa tumbo pamoja na Kuharisha?

UHUSIANO KATI YA HOFU AU WASIWASI NA TUMBO LA KUHARISHA

Bila shaka umewahi kusikia au hata wewe mwenyewe tatizo hili limewahi kukukuta,

Baadhi ya watu wakipata hofu au kuingiwa na wasi wasi juu ya jambo flani hupata maumivu makali ya tumbo au tumbo kuvurugika pamoja na kuharisha

Je kuna uhusiano gani kati ya hofu au Wasiwasi na mtu kupata mvurugiko wa tumbo pamoja na Kuharisha?

FAHAMU HII;

Kutokana na Jumuiya ya marekani inayojishuhulisha na mambo ya Hofu,wasiwasi pamoja na Msongo wa mawazo yaani “ANXIETY AND DEPRESSION ASSOCIATION OF AMERICA(ADAA)” ilisema kwamba;

Wakati mtu akiwa na hofu/wasiwasi mwili wake huzalisha vichocheo pamoja na Kemikali ambazo zinaingia kwenye mfumo wa umeng’enyaji wa chakula yaani Digestive tract,

na kuanza kuwaharibu wale bacteria Wazuri au gut Flora, hali ambayo hupelekea mabadiliko makubwa ya gafla mwilini,

kisha mtu kuanza kupata hali kama vile; tumbo kujaa gesi,tumbo kuuma au Mvurugiko wa tumbo pamoja na kuharisha

VITU AMBAVYO HUWEZA KULETA HOFU AU WASIWASI KWA MTU NI PAMOJA NA;

✓ matukio mabaya kwenye maisha kama vile; Ajali, misiba, n.k

✓ hofu na wasawasi wa mitihani kwa wanafunzi

✓ mtu kukabwa na kuibiwa

✓ mtu kutishiwa maisha

✓ mtu kufanyiwa vitendo vya kinyama kama vile; kubakwa, kulawitiwa n.k

✓ ugomvi na mifarakano ya kimahusiano na ndoa

✓ hali mbaya ya kiuchumi ikiwa ni pamoja na mtu kuwa na madeni kila kona

N.K

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.