Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Madhara ya Kung’ata,kula au Kuuma Kucha zako na JINSI ya kuacha Tabia hii

Madhara ya Kung’ata,kula au Kuuma Kucha zako na JINSI ya kuacha Tabia hii

Kando na kuharibu ngozi na kucha, hii pia inaweza kuumiza meno yako na kusababisha maambukizi.Soma Zaidi hapa…

MADHARA YA KULA KUCHA

kumbuka unavyokula kucha unaweza kuleta shida kwenye kucha ila wakati mwingine ni mpaka kwenye nyama au tissues za vidoleni,

– Unaweza kupata vidonda au michubuko kwenye kucha au kuzunguka ngozi ya vidole, Vidonda hivi huweza kupelekea maumivu, damu kuvuja kwenye kidole n.k

– Kula kucha kunasababisha kucha kutokuwa na muonekano mzuri(abnormal-looking nails)

– Kuwa kwenye hatari ya kupata fangasi(fungal Infections) hasa kwenye eneo la Nail Plate pamoja na kuzunguka ngozi

– Kupata magonjwa mengine kutokana na vimelea vya magonjwa kama vile Bacteria pamoja na Virusi kutoka vidoleni kwenda mdomoni wakati unakula kucha.

– Unaweza kusababisha madhara mengine kwenye meno kama vile; meno kuchimba,mpangilio mbaya au tatizo la dental resorption

– Kupata maumivu kama vile temporomandibular joint pain pamoja na dysfunction

– Kusababisha michubuko mdomoni, kwenye fizi za meno n.k

– Pia tabia hii ya kula kucha inaweza kuongeza hatari ya wewe kupata maambukizi kama vile stomach and intestinal infections. N.K

JINSI YA KUACHA TABIA HII YA KULA KUCHA

Kama tunavyojua tabia sio kitu ambacho hutokea ndani ya siku moja,hivo hata kuacha kwake pia huweza kuwa ni mchakato endelevu. Ukiona njia ya kwanza haifanyi kazi jaribu ya pili, mpaka upate matokeo unayoyataka.

1. Hakikisha unakata kucha zako vizuri, moja ya sababu ambazo hupelekea kuanza kula kucha ni pale unapoona kucha zako ni ndefu, hivo hakikisha hukai na kucha ndefu zikate vizuri kila wakati zinapokua.

2. Jenga utaratibu wa kutunza kucha zako na kuhakikisha zinakuwa na muonekano mzuri,

Huwezi kung’ata kucha kama unatamani kucha zako ziwe na muonekano mzuri

3. Na kwa wale ambao wanapaka rangi kucha, hii inaweza kuzuia wewe kula kucha zako, kwa kuogopa kuharibu muonekano,

lakini pia kuogopa kula rangi mdomoni, na wakati mwingine mbali na kwamba rangi ina makemikali, pia huleta ladha mbaya mdomoni.

4. Dhibiti matatizo mengine kama vile Woga, wasi wasi, msongo wa mawazo n.k

5. Hakikisha mikono yako inakuwa bzy kwa kufanya vitu mbali mbali, moja ya vitu ambavyo huweza kukushawishi wewe kuanza kula kucha, ni mikono yako kukosa chakufanya.

6. Kama pia imekuwa too much,sio vibaya kufanya vipimo ikiwemo Vipimo vya afya ya akili

UKIONA MAMBO HAYA ONANA NA WATAALAM WA AFYA MAPEMA ZAIDI

– Kucha imeanza kuota pembeni au umepata tatizo la ingrown nails

– Maambukizi ya kwenye ngozi au kucha, kuwa na vidonda ambavyo haviponi n.k

– Kucha kupoteza rangi yake ya asili(nail discoloration)

– Kuvuja damu kuzunguka kwenye kucha ambayo inatoka mfululizo

– Kucha kuacha kuota tena au kuacha kukua, kucha kutoka kabsa n.k

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.