Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

jinsi ya kujikinga na saratani ya matiti,Soma hapa

jinsi ya kujikinga na saratani ya matiti,Soma hapa….

Ni muhimu sana kufahamu baadhi ya Njia za kupunguza hatari ya Kupata Saratani ya Matiti,

Japokuwa hata Wanaume hupatwa na SARATANI ya Matiti ila Kwa Wanawake Idadi ni kubwa zaidi ikilinganishwa na Wanaume.

Na kwa Mujibu wa kitengo cha udhibiti na Kuzuia magonjwa yaani Centers for diseases control and Prevention(CDC-Cancer) wanasema;

Kila Mwanamke Mmoja(1) kati ya Nane(8) nchini Marekani hupata shida ya SARATANI ya Matiti katika kipindi cha MAISHA yake.

(CDC-Cancer):

“About 1 in 8 women in America will get BreastCancer during her lifetime”.

JINSI YA KUPUNGUZA HATARI YA KUPATA SARATANI YA MATITI

Kuna sababu nyingi ambazo huweza kuongeza uwezekano wa mtu kupata Saratani hii ya Matiti na zingine hatuwezi kuzizuia kama vile; mtu kuwa na umri mkubwa zaidi, historia kwenye Familia yako n.k

Lakini kwa Kutumia Njia hizi hapa Chini,tunaweza Kupunguza hatari ya Kupata Saratani ya Matiti;

– Hakikisha unadhibiti tatizo la kuwa na Uzito Mkubwa au hakikisha unakuwa na Uzito ambao ni Salama Kiafya

– Fanya Mazoezi ya Mwili Mara kwa Mara

– Epuka matumizi ya Pombe kupita kiasi

– Epuka Uvutaji wa Sigara

– Tumia Dawa zozote zenye vichocheo yaani hormone replacement therapy au dawa kama za kupanga Uzazi-oral contraceptives (birth control pills), kwa Maelekezo ya kina kutoka kwa Wataalam wa afya,

epuka matumizi ya kiholela kwa Dawa kama hizi zenye vichocheo ndani yake.

– Kwa Mwanamke mwenye mtoto anayenyonya, hakikisha unamnyonyesha mtoto kadri iwezekanavyo,

Tafiti zinaonyesha,Kunyonyesha mtoto kwa kiwango kinachotakiwa,humpunguzia Mwanamke hatari ya kupata Saratani ya Matiti.

– Kama upo kwenye Familia ambapo kuna shida hii ya Watu kuugua Saratani ya Matiti, ongea na wataalam wa afya wabobezi kwenye eneo hili la SARATANI, ili wakupe njia angalau za kukusaidia kupunguza hatari ya wewe kuugua Saratani hii.

– Jenga Tabia ya Kufanya checkup Mara kwa Mara, hasa pale unapoona hali ya tofauti kwenye matiti yako.

MAMBO YANAYOONGEZA HATARI YA KUPATA SARATANI YA MATITI

(1) Jinsi ya kike,wapo kwenye hatari Zaidi

(2) Kuanza hedhi katika umri mdogo.

(3) Kukoma siku katika umri mkubwa

(4) Kutozaa kabisa.

(5) Kutonyonyesha kabisa au kunyonyesha kwa muda mfupi.

(6) Utumiaji mafuta mengi katika chakula.

(7) Kutokufanya mazoezi ya mara kwa mara.

(8) Unene kupita kiasi

(9) Uvutaji sigara.

(10) Utumiaji wa pombe kupita kiasi.

(11) Historia ya saratani ya matiti katika familia.

SOMA ZAIDI: Saratani ya MATITI,dalili zake n.k

#BreastCancerAwarenessMonth

 

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.