Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Tatizo la Ovarian cysts,Chanzo,Dalili na Tiba yake

Tatizo la Ovarian cysts,Chanzo,Dalili na Tiba yake

Ovarian cysts ni vivimbe Maji ambavyo huhusisha vifuko vilivyojaa maji maji(fluid) ndani ya Ovaries au kwenye surface yake,

Tatizo hili la Ovarian cysts hutokea sana kwa wanawake wengi, na mara nyingi unaweza usipate shida yoyote au dalili, na asilimia kubwa huisha vyenyewe bila hata matibabu yoyote ndani ya Miezi michache.

Lakini wakati mwingine ovarian cysts huweza kubanwa na kupasuka kwa ndani, Hii ikitokea huweza kuleta madhara zaidi,

DALILI ZA TATIZO LA OVARIAN CYSTS

Asilimia kubwa Mwanamke mwenye tatizo la ovarian cysts hapati dalili yoyote na tatizo linaisha lenyewe, Lakini endapo vivimbe Maji hivi ni vikubwa(large ovarian cyst),

Mwanamke huweza kupata dalili kama hizi;

– Maumivu ya kiuno ambayo huja na kuondoka mara kwa mara,

– Kupata maumivu chini ya kitovu kuelekea upande Mmoja

– Kuhisi hali ya tumbo kujaa,Mgandamizo au Uzito tumboni

– Na wakati mwingine tumbo Kuvimba

MUONE DAKTARI HARAKA ENDAPO;

• Unapata maumivu ya gafla na makali sana ya tumbo

• Unapata maumivu makali pamoja na HOMA au KUTAPIKA

• Unashindwa kupumua, Unapumua kwa haraka n.k

CHANZO CHA TATIZO LA OVARIAN CYSTS

Asilimia kubwa ya shida hii ni matokeo ya Mzunguko wako wa hedhi(menstrual cycle). ambapo kwa kitaalam tunaita functional cysts,

Japo kuna aina nyingine za vivimbe Maji(cysts) ila ni nadra kutokea ukilinganisha na hii.

Kwa kawaida vifuko vya Mayai yaani OVARIES hukua small cysts Kwa kila MWEZI ambazo hujulikana kama follicles.

Follicles huzalisha vichocheo aina ya estrogen pamoja na progesterone,Kisha hupasuka na kutoa Yai wakati wa Ovulation,

Sasa basi, hizi follicles ambazo hukua kila mwezi ndyo hutengeneza kitu kinaitwa functional cyst/Ovarian cysts.

Na kwa asilimia kubwa hazisababishi maumivu yoyote na hupotea zenyewe ndani ya Mizunguko 2 mpaka 3 ya hedhi(menstrual cycles),

Ila tatizo hutokea na kuleta madhara kama maumivu makali ya tumbo pamoja na dalili zingine wakati Ovarian cysts zikiwa Kubwa zaidi.

VITU HIVI HUONGEZA HATARI YA MWANAMKE KUPATA SHIDA YA OVARIAN CYSTS

– matatizo ya vichocheo mwilini(Hormones), ambayo husababishwa na vitu mbali mbali kama vile;

Matumizi ya dawa za Uzazi, hasa ambazo husababisha Mwanamke kupevusha mayai kama vile clomiphene citrate au letrozole

– Ujauzito,Wakati mwingine follicles ambazo zimetengenezwa wakati wa Ovulation huendelea kubaki kwenye Ovaries kipindi chote cha Ujauzito, hali ambayo hupelekea kukua Zaidi

– Tatizo la Endometriosis, ambalo huweza kusababisha baadhi ya Tissues kujishikiza kwenye Ovaries kisha kutengeneza Vivimbe Maji au Cysts

– Mwanamke kupata maambukizi makali sana eneo la Pelvic, hasa pale ambapo maambukizi haya yatasambaa mpaka kwenye vifuko vya Mayai(Ovaries)

– Kuwa na shida hii huko Nyuma, kama umeshawahi kuwa na Ovarian cyst moja,basi unaweza kuwa na zaidi pia.

MATIBABU YA OVARIAN CYSTS

Tiba hutegemea na Umri,aina pamoja na Size(Ukubwa) wa Ovarian cysts,

Hivo basi mambo haya hapa huweza kufanyika kwa Mgonjwa;

1. Kuendelea kusubiri na kufanyiwa uchanguzi mara kwa mara ili kuona kama Cysts zinaondoka zenyewe baada ya miezi michache, Hivo utafanyiwa vipimo kama Ultrasound mara kwa mara

2. Matumizi ya dawa

3. Na Mwisho Upasuaji, kuondoa Cysts hizi

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

4 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.