Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Wanawake ambao wapo kwenye hatari ya Kuzaa Watoto Njiti(Premature babies)

Wanawake ambao wapo kwenye hatari ya Kuzaa Watoto Njiti(Premature babies)

Watoto Njiti yaani Premature babies, ni watoto ambao huzaliwa kabla ya Wakati, Mfano kuanzia wiki 28 na kabla ya Wiki 37 za Ujauzito,

WANAWAKE AMBAO WAPO KWENYE HATARI YA KUZAA WATOTO NJITI NI PAMOJA NA;

1. Wale ambao wamewahi kuzaa watoto njiti kwenye mimba zilizotangulia

2. Wanawake Wajawazito ambao wana Mimba ya Mapacha wawili(twins), watatu(triplets) au zaidi

3. Wanawake ambao huzaa kwenye kipindi cha kabla ya Miezi 6 toka wajifungue mimba iliyotangulia

4. Wanawake wanaotumia tumbaku(tobacco uses) au dawa zingine za kulevyia

5. Wanawake wanaobeba mimba kwa Njia ya vitro fertilization

6. Wanawake wenye matatizo ya kizazi kama vile uvimbe n.k

7. Wanawake wenye matatizo kwenye mlango wa kizazi(Cervix), kama vile tatizo la Mlango wa kizazi(Cervix) kushindwa kufunga vizuri n.k

8. Wanawake wenye matatizo kwenye Kondo la Nyuma yaani Placenta

9. Wanawake wanaopatwa na matatizo mbali mbali kipindi cha Ujauzito kama vile Kifafa cha Mimba N.k,

10. Wanawake wanaovuta Sigara

11. Mwanamke kupata baadhi ya maambukizi hasa hasa yanaogusa amniotic fluid au lower genital tract

12. Mwanamke kuwa na matatizo kama vile Presha kuwa Juu Sana, Kuwa na tatizo la Kisukari n.k

13. Mwanamke kuwa Mnene sana,Uzito Mkubwa sana au Kuwa na Uzito Mdogo sana kabla ya Kubeba Mimba

14. Mwanamke kupatwa na matukio ambayo humpa sana msongo wa mawazo kama vile; vifo vya watu wake wa karibu ambao huwapenda sana, ugomvi wa kifamilia n.k

15. Mwanamke kuumia kwa namna yoyote kama vile; Kupata ajali, kupigwa n.k

16. Wanawake ambao wametoa Mimba mara nyingi(Multiple miscarriages au abortions) n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.