Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Baadhi ya mambo ya kufanya kama Una Shida ya kupata CHOO KIGUMU

Baadhi ya mambo ya kufanya kama Una Shida ya kupata CHOO KIGUMU

Sababu mbali mbali huweza kuchangia shida ya mtu kupata choo Kigumu mfano;

• Aina ya chakula unachokula- mfano kula Mlo wenye nyuzi nyuzi kwa kiwango kidogo sana-low fibers,

• Matumizi ya baadhi ya Dawa,

• Kuwa Mjamzito,Mabadiliko ya vichocheo mwilini hasa wakati wa Ujauzito huweza kupelekea tatizo la kupata choo kigumu

• Kutokufanya mazoezi,

• kubana Haja kwa Muda mrefu bila Kujisaidia kulingana na mazingira Uliyopo n.k,

FANYA HAYA;

– Epuka kubana haja kubwa kwa muda mrefu mara kwa mara, kukaa muda mrefu bila kwenda chooni kujisaidia wakati unahisi Kujisaidia,

Hali ambayo hupelekea maji kuendelea kufyonzwa kwa kiasi kikubwa na kuleta ukavu kwenye haja kubwa

– Kutokunywa maji mengi kwa siku, unashauriwa kunywa maji angalau lita 2.5 mpaka 3 za maji kwa siku

– Epuka kula Mlo wenye nyuzi nyuzi kwa kiwango kidogo sana-low fibers, badala yake kula vyakula vyenye nyuzi nyuzi kwa kiwango kikubwa,mfano karanga, nafaka isiyokobolewa, maharage, mboga za majani n.k

Lakini pia kula matunda kama vile; parachichi,papai n.k

– Fanya Mazoezi mbali mbali ya Mwili

– Pia epuka Msongo wa mawazo, Watu wanaopata msongo mkubwa wa mawazo huharibu mpangilio wa homone zao pamoja na kuathiri uzalishaji wa visambaza taarifa kwenye mwili na hivo kusababisha shida kwenye misuli, kuathiri ufanyaji kazi wa enyzmes ambazo husaidia kumeng’enya chakula.

– Tumia kinywaji cha uvuguvugu: kama una tatizo la constipation jaribu kutumia chai ya moto asubuhi, au tumia maji yaliyochanganywa na limau n.k

– Epuka matumizi ya Pombe au
Vinjwaji vyenya caffeine kwa wingi kama kahawa na baadhi ya chai

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.