Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Chanzo cha tatizo la kutokuhisi harufu ya kitu chochote au Kupoteza hisia ya harufu(Anosmia)

Chanzo cha tatizo la kutokuhisi harufu ya kitu chochote au Kupoteza hisia ya harufu(Anosmia)

Tatizo hili la kupoteza uwezo wa kuhisi harufu ya kitu chochote kwa kitaalam hujulikana kama Anosmia,

Na hapa nimekuoorodheshea baadhi ya Sababu mbali mbali ambazo huweza kusababisha tatizo hili;

1. Maambukizi ya Vimelea mbali mbali vya magonjwa kama vile bacteria au virusi eneo la Puani, Mfano kwenye tatizo la MAFUA, ambapo husababishwa na virusi aina ya INFLUENZA VIRUS

2. Tatizo la Allergy/Mzio, mfano; Hay fever(Homa ya nyasi), ambapo hapa huhusisha mtu kuwa na allergic reactions dhidi ya vitu kama vile; vumbi,Pollens za mimea n.k

3.Pia tatizo la kupoteza uwezo wa kuhisi harufu linaweza kuwa na uhusiano na vitu hivi;

– Kuwa na Tatizo la Kisukari(diabetes)

– Tatizo lolote linoweza kupelekea pua kuziba kama vile; Nasal Polyps n.k

– Maambukizi kama Sinus Infections(Sinusitis)

– Tatizo la Uzito kuzidi(Overweight/Obesity)

– Ugonjwa wa Alzheimers

– Matumizi ya baadhi ya dawa,mfano jamii ya antibiotics au antihistamines

– Uvutaji wa Sigara

– Matatizo ya vichocheo mwilini(Hormonal changes)

– Matumizi ya Pombe kwa Muda mrefu(Long-term alcoholism)

– Tatizo la Brain tumors, Brain Injury n.k

– Tatizo la Multiple Sclerosis

– Kuwa kwenye mazingira ya baadhi ya Kemikali kwa muda mrefu, hali ambayo husababisha kemikali hizi kupenya kupitia Puani

– Tatizo la Utapiamlo na Upungufu wa Vitamins(Malnutrition&Vitamins defficiency)

– Tatizo la presha kuwa juu(High blood pressure)

– Tatizo la Kiharusi(STROKE)

– Tatizo la Kifafa(Epilepsy)

– Huduma ya Mionzi kwa muda mrefu(Radiation therapy)

– Kufanyiwa Upasuaji unaohusu Ubongo(Brain surgery) N.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.