Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Malezi ya Mtoto,Kama Mzazi au Mlezi hakikisha unafanya haya kwa Mtoto

Malezi ya Mtoto,Kama Mzazi au Mlezi hakikisha unafanya haya kwa Mtoto

Moja ya changamoto kubwa tuliyonayo kwa Kipindi cha Sasa ni Pamoja na Hili la Malezi ya Watoto,

tumekuwa buzy mno na kazi kiasi kwamba tumesahau kabsa Kuwa na Muda na watoto wetu.

Nakukumbusha,Jitahidi kufanya Vitu Hivi kwa Mtoto wako;

Kulingana na Umri wake

1. Hakikisha unapata muda wa kutosha kukaa na mtoto wako,

usimuachie Msichana wa kazi kila kitu mpaka malezi ya mtoto akulelee yeye.

2. Hakikisha mtoto wako anapata chakula,maziwa n.k kila wakati anapohitaji kulingana na umri wake,

Wazazi wengi hata kama wapo karibu na watoto wadogo wanaonyonya,huwanyonyesha muda wanaotaka au kupanga wao na sio kila wakati mtoto anapohitaji,

Unashauriwa kumnyonyesha mtoto na kumpa chakula kila muda anapotaka yeye sio muda unaopanga wewe.

3. Hakikisha unapata muda wa kukaa na kuongea na mtoto wako mambo mbali mbali,jenga ukaribu sana na mtoto wako(Strong Bonding) ili awe rafiki na muwazi kwako kwa kila kitu kinachomsibu,

tumeshuhudia watoto wengi kufanyiwa vitendo vya Ukatili na hata wazazi hawajui,

Kwani hawapo karibu na watoto,hivo mtoto hata kuongea na wewe anaogopa.

Mfanye mtoto kuwa rafiki wa karibu ambaye anaweza mueleza kila kitu pasipo uoga.

4. Kama ni mtoto wa Shule,hakikisha unapata muda wa kuongea naye kuhusu maendeleo yake ya Shule,

Mfundishe vile ambavyo unapaswa kumfundisha ili kumjenga zaidi kimasomo,

Tenga muda wa kukagua madaftari ya mtoto,ongea na mtoto,mfundishe n.k( kumbuka wewe pia ni mwalimu wa mtoto wako)

5. Mfundishe mtoto maadili mema,mfundishe mtoto maadili ya DINI na Kumheshimu MUNGU, ili kumjengea MTOTO hofu ya MUNGU

• Kama ni MKRISTO,hakikisha unamjenga kwenye maadili ya Kikiristo

• kama ni MUISLAM, mjenge kwenye maadili ya Kiislam n.k

KUMBUKA; Mtu bora na Mwenye maadili mema huanza kutengenezwa ndani ya Familia yake

6. Mfundishe Mtoto maisha, na kama amefikia umri wa kuweza kufanya kazi ndogo ndogo,anza naye ili kumjengea msingi wa Kujitegemea na kujishughulisha Mapema,

Epuka kumfanyia mtoto wako kila kitu eti kwa vile unampenda,

Mfundishe mtoto wako kazi mbali mbali kama vile kufua,Kupika,kuosha vyombo, Kulima n.k

7. Mlee Mtoto kwenye Njia Ipasayo, Naye hataiyacha hata atakapokua Mtu mzima.

Asante kwa MALEZI BORA kwa Watoto Wetu….,

Nimatumaini yangu kwamba angalau Umepata kitu kupitia makala hii.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.