Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Mishumaa kuongeza hatari ya Mzio/Allergies kwa Watu

Mishumaa kuongeza hatari ya Mzio/Allergies kwa Watu

Fahamu mambo haya yatakusaidia kwenye afya yako,

Leo kwenye afyaclass Lifestyles tumegusa vitu viwili;

(1) Matumizi ya Mishumaa

(2) Na Wanaofanya kazi zinazohusisha Unga yaani Waokaji

MISHUMAA:

Aina ya Mishumaa inayojulikana zaidi, inatengenezwa au inatokana na mafuta ya taa yaani petroleum-based paraffin,

Aina hii ya Mishumaa hutoa kemikali hewani ambayo inaweza kuongeza hatari au athari za mzio(Allergies) kwako,

Vile vile huweza kuongeza hatari ya matatizo ya kupumua kama vile pumu, na hata saratani.

Matumizi ya mara kwa mara pengine ni sawa, lakini kuwasha kila siku Mishumaa huenda lisiwe wazo zuri kwa muda mrefu.

Kwa chaguo salama, jaribu mishumaa iliyotengenezwa kwa nta au soya, na uhakikishe kuwa kuna mtiririko mzuri wa hewa kila unapochoma au Kutumia Mishumaa.

UNGA:

Watu wanaofanya kazi ya Uokaji huweza kupata shida ya kukohoa, kupumua, na kukosa Pumzi zaidi kuliko wengine.

Huenda ni kutokana na kazi ya kutumia unga hali ambayo husabisha kuvuta Unga na kuingia kwenye mfumo wa hewa.

Na wakati mwingine athari huweza kuonekana mpaka nyumbani kwa familia za baadhi ya Waokaji, hii huweza kutokana na Nguo walizovaa,Ngozi, au nywele kushika Vumbi La Unga pasipo kujua.

Hali hii ya kuvuta Unga huweza kusababisha madhara kwenye mfumo wa hewa, kuleta mafua,kikohozi,shida ya kupumua, na wakati mwingine kuharibu kabsa mapafu,kuleta tatizo la Pumu n.k

Kama unafanya kazi za aina Hii, hakikisha unavaa vitu vya Kujikinga Kama Masks(Barakoa), badilisha nguo na acha nguo za kazini usirudi nazo nyumbani,Oga n.k

#afyaclass lifestyle

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.