Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Mwanamke mwenye Saratani ya Titi Moja yupo kwenye hatari ya kupata Saratani kwenye titi Lingine

Mwanamke mwenye Saratani ya Titi Moja yupo kwenye hatari ya kupata Saratani kwenye titi Lingine

Baadhi ya Tafiti zinaonyesha kwa Mwanamke mwenye Saratani ya Titi Moja, yupo kwenye hatari zaidi ya kupata Saratani na kwenye titi la Pili,

Na hii hutokea kama Mwanamke huyo ni carriers wa mabadiliko maalum ya kigenetics ambayo yamepelekea kupata Saratani kwenye titi lake la Kwanza(specific genetic changes),

Hii ni kutokana na utafiti ambao ulifanywa na “Mayo Clinic Comprehensive Cancer Center” kisha matokeo ya utafiti huu kuchapishwa kwenye jarida la “the Journal of Clinical Oncology”.

Lengo likiwa ni kupanua wigo wa kiuchunguzi kwa wagonjwa wenye Saratani ya Matiti yaani breast cancer screening na kutambua Sababu zote hatarishi ambazo huweza kuongeza hatari ya Mwanamke kupata Saratani ya Matiti na kupata Tiba mapema,

Utafiti huu ulihusisha Wanawake 15,104 ambao wapo kwenye kundi la Cancer Risk Estimates Related to Susceptibility (CARRIERS) consortium.

Matokeo yalionyesha kwamba, Wagojwa wote ambao walikuwa na mabadiliko haya ya kigenetics hasa wenye germline BRCA1, BRCA2 or CHEK2 mutation wana hatari mara mbili zaidi ya kupata Saratani kwenye matiti yote mawili,

Hali hii kwa Kitaalam hujulikana kama contralateral breast cancer.

Pia Matokeo yalionyesha kwamba, wanawake ambao wanakaribia kwenye Ukomo wa Hedhi(premenopausal women) na wanamabadiliko haya ya Kigenetics wapo kwenye hatari zaidi ya kupata Saratani kwenye Matiti yote mawili ikilinganishwa na wanawake ambao tayari walishafikia kipindi cha Ukomo wa Hedhi(Post-menopause women).

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.