Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Tips Sita(6) za kukusaidia Kulinda FIGO zako

Tips Sita(6) za kukusaidia Kulinda FIGO zako

Moja ya Vitu ambavyo unatakiwa kulinda Sana ni Pamoja na FIGO,

Leo nimekuandalia Tips Sita(6) za kukusaidia kulinda Figo Zako, Soma zaidi hapa..!!

(1) Hakikisha unadhibiti Uzito wa Mwili na epuka kuwa na Uzito mkubwa kupita kiasi

Kumbuka Uzito mkubwa ni chanzo kikubwa cha kukaribisha magonjwa mengine kama vile Presha,kisukari,magonjwa ya moyo n.k ambavyo vyote hivi huathiri pia afya ya Figo

(2) Kunywa Maji mengi kila siku,

Unywaji wa maji mengi kila siku husaidia sana FIGO kuondoa Sumu kwenye Damu, na hii huleta afya kwa mwili mzima pamoja na Figo pia

(3) Epuka Kuoverdose dawa, hasa dawa jamii ya Non-Steroidal anti-Inflammatory(NSAIDs) kama vile Ibuprofen n.k

Tumia dawa hizi kwa uangalifu, epuka Overdosing pamoja na matumizi ya muda mrefu sana ya dawa kama hizi

(4) Fanya checkup ya Figo mara kwa mara, hasa kama umetokea kwenye Familia yenye historia ya magonjwa ya Figo kushindwa kufanya kazi(kidney failure),Kisukari,Presha n.k

(5) Kula mlo kamili, epuka ulaji wa mafuta Mengi n.k

Kula mlo ambayo hautakuweka kwenye hatari ya kupata magonjwa kama vile;Presha,Kisukari,magonjwa ya moyo,Shida ya Uzito mkubwa n.k

(6) Epuka Uvutaji wa Sigara Pamoja na Kudhibiti Matumizi ya Pombe.

KUMBUKA: Matibabu ya FIGO yana Garama sana,LINDA FIGO Zako..!!!

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.