Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

MWANAMKE Fanya Uchunguzi wa Saratani ya Mlango wa Kizazi Mara Kwa Mara

MWANAMKE Fanya Uchunguzi wa Saratani ya Mlango wa Kizazi Mara Kwa Mara,

Faida za Kufanya Uchunguzi wa Saratani ya mlango wa Kizazi (Cervical cancer Screening) mara kwa mara ni kubwa mno kwa Wanawake,

Kufanya Checkup kama hizi mara kwa mara itamsaidia Mwanamke ambaye tayari ana Saratani ya Mlango wa Kizazi kugundulika mapema na kupata Tiba,

KUMBUKA: Ni rahisi kupata Tiba na kupona kabsa kama Saratani ya mlango wa Kizazi(Cervical cancer) imegundulika mapema na Kuanza tiba mapema.

Wanawake ambao wapo Kwenye Hatari ya Kupata saratani ya shingo ya Kizazi,

Kwa Ujumla wanawake wote wapo kwenye hatari ya Kupata Saratani ya shingo ya Kizazi, ila kundi hili hapa Chini Lipo kwenye hatari zaidi.

KUNDI LILILOPO KATIKA HATARI YA KUPATA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

➖ Wanawake wanaoanza kushiri tendo la Ndoa au mapenzi wakiwa na umri mdogo mfano kabla ya miaka 18 au 20.
➖ Wanawake wenye wapenzi wengi yaani Multiple sexual parteners
➖ Wanawake wenye Umri mkubwa mfano miaka 50 na kwenda mbele,
Saratani hii huweza kuathiri zaidi Wanawake Kuanzia Miaka 35 mpaka 49
➖ Wanawake wanaozaa katika umri mkubwa mfano miaka 48.
➖ Wanawake wanaotumia dawa zozote zinazohusu kuongeza uzalishaji wa seli hai za Mwili.

➖ Wanawake Wenye Maambukizi ya Ukimwi(HIV/AIDS) au wanawake wenye magonjwa yoyote ambayo huweza kuathiri mfumo wa Kinga ya Mwili

➖ Wanawake wanaoshambuliwa na Kirusi cha Human papilloma virus(HPV) mara kwa mara

➖ Wanawake wanaovuta Sigara

➖ Wanawake wanaozaa watoto wengi

➖ Wanawake wanaotumia vidonge vya Uzazi wa Mpango(birth control Pills) Kwa Muda Mrefu zaidi, Mfano Kwa Miaka 3,5 au Zaidi.

DALILI NA VIASHIRIA VYA KUWA NA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI.

SARATANI NI NINI?
Saratani ni hali ya ukuaji wa seli hai za mwili usio wakawaida au ulizidi kiwango,Kwahyo basi, Saratani ya shingo ya kizazi ni ukuaji usio wa kawaida wa seli hai zilizopo au zinazounda eneo la shingo ya kizazi.

Chanzo cha Saratani ya Shingo ya Kizazi

Saratani ya Kizazi au saratani ya shingo ya kizazi husababishwa na Kirusi aitwaye HUMAN PAPILLOMA VIRUS (HPV).
kirusi huyu ndyo Mhusika mkuu wa Tatizo hili ambapo kitaalam tatizo hili la Saratani ya shingo ya Kizazi hujulikana kama “cervical Cancer”
?DALILI ZA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

Saratani ya shingo ya kizazi katika hatua za awali haina dalili au viashiria vyovyote.

– Kutokwa na damu katika tupu ya mwanamke (vagina) ambayo sio ya kawaida. Damu hii inaweza kuwa matone, au damu inayotoka katikati ya mzunguko wa hedhi (yaani baada ya hedhi kabla ya hedhi inayofuata) au damu itokayo kwa mwanamke ambae ameacha kupata hedhi.

– Kutokwa na damu baada ya kujamiana baada ya tendo la ndoa.

– Maumivu wakati wa kujamiana.

Dalili za saratani iliyosambaa ni kama zifuatavyo

– Kutokwa na majimaji ukeni kusiko kawaida yenye harufu na maumivu ya tumbo chini ya kitovu.

– Kupungua kwa hamu ya kula

– Kupungua uzito

– Kuhisi uchovu

– Maumivu ya nyonga

– Maumivu kwenye mgongo

– Maumivu ya mguu

– Mguu mmoja kuvimba

– Kutokwa na damu nyingi kwenye tupu ya mwanamke

– Kuvunjika mifupa (bone fractures)

– Kutokwa na mkojo au kinyesi kwenye tupu ya mbele ya mwanamke.

MADHARA YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

(1) Kupoteza maisha kwa Mwanamke
(2) Kutolewa kizazi chote na kupoteza uwezo wa mwanamke kuzaa tena
(3) Kuvuja damu na kupata maumivu makali wakati wa tendo la ndoa
(4) Kutokwa na harufu kama ya kitu kilichooza Ukeni

MATIBABU YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI

Endapo tatizo hili litakugundulika katika stage za mwanzoni kabsa,mwanamke atapata tiba na atapona kabsa.Lakini kama akachelewa na saratani hiii au kansa hii ikafika stage iv ni ngumu kupona.
Kwahyo basi kuna umuhimu sna wa Kujichunguka kila wakati na pale unapoona mabadiliko yoyote mwilin,wahi hosptal kwa ajili ya uchunguzi na matibabu.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.