Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Matumizi makubwa ya dawa za usingizi na mtu kupata tatizo la kupoteza kumbu kumbu(dementia) hapo baadaye

Matumizi makubwa ya dawa za usingizi na mtu kupata tatizo la kupoteza kumbu kumbu(dementia) hapo baadaye

Utafiti mpya umehusisha matumizi makubwa ya dawa za usingizi na mtu kupata tatizo la kupoteza kumbu kumbu(dementia) hapo baadaye.

Utafiti mpya uliochapishwa hivi karibuni kwenye jarida la Journal of Alzheimer’s Disease umehusisha matumizi makubwa ya dawa za usingizi na ongezeko la ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu yaani dementia hapo baadaye.

Watafiti walihusisha zaidi ya watu wazima 3,000 wenye wastani wa umri wa miaka 74 wanaotumia dawa za Usingizi, wasio na shida yoyote ya kupoteza kumbukumbu(dementia),

Utafiti huo wa kuangalia uhusiano kati ya matumizi makubwa ya dawa za Usingizi na uwepo wa tatizo la Kupoteza kumbukumbu(dementia) ulijumuisha asilimia 58% ya wazungu na asilimia 42% washiriki Weusi.

Katika kipindi cha utafiti, ambacho kilidumu miaka 15, moja ya tano ya washiriki walipata shida ya Kupoteza kumbu kumbu(dementia).

Hivo kwa Mujibu wa Matokeo haya inaonyesha ukitumia dawa za Kukusaidia upate Usingizi kwa kiwango kikubwa mfano wa dawa kama Ambien (zolpidem),Valium, (diazepam, a benzodiazepine)
unaweza kupata tatizo la kupoteza kumbukumbu hapo baadae.

Hitimisho;

Kutokana na utafiti huu, kuna Uhusiano wa Matumizi ya dawa za usingizi na mtu kupata tatizo la kupoteza kumbu kumbu(dementia) hapo baadaye,

Hivo unashauriwa kuepuka matumizi ya dawa za Usingizi kwa Kiwango kikubwa, badala yake Ongea na wataalam wa afya wakupe Njia sahihi za kukusaidia upate Usingizi wa kutosha,kama una tatizo la Kukosa Usingizi.

• SOMA Pia baadhi ya Vidokezo vya Kukusaidia Upate Usingizi mzuri

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.