Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Njia za kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya kupumua kama vile pneumonia

Njia za kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya kupumua kama vile pneumonia

Kuna Magonjwa mbali mbali yanayohusu mfumo wa Upumuaji(respiratory diseases),

Na katika makala hii,tumechambua Zaidi kuhusu Njia za kupunguza hatari ya Kupata magonjwa ya kupumua ambayo hutokea kwa watu wengi Zaidi, kwa kitaalam tunasema common respiratory diseases.

Magonjwa ya kupumua ni kama vile;

  • Ugonjwa wa pneumonia
  • Ugonjwa wa Asthma.
  • Tatizo la pneumothorax au atelectasis
  • Tatizo la bronchitis
  • chronic obstructive pulmonary disease (COPD)
  • Kansa ya Mapafu(Lung cancer)
  • Tuberculosis(TB)
  • Tatizo la pulmonary edema n.k

Njia za kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya kupumua

Kuna Njia mbali mbali za kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya kupumua,na njia hizo ni kama vile;

– Kuepuka kukaa kwenye maeneo ya Msongamano wa watu wengi,

Unaweza kupata vimelea mbali mbali vya magonjwa ya Kupumua kama vile Virus vya mafua(Influenza) n.k,kwa kuwa karibu sana na watu hasa wenye magonjwa kama haya.

Hivo basi,kuepuka kukaa kwenye maeneo yenye msongamano mkubwa wa watu ni mojawapo ya Njia za kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya kupumua.

– Funga mdomo wakati wa kukohoa au kupiga chafya,

Vimelea vya magonjwa ya kupumua kama vile Tuberculosis(TB) vinaweza kusambaa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kupitia vitone vidogo vidogo ambavyo huruka hewani kwenye hewa baada ya mtu mwenye vimelea hivi kukohoa au kupiga chafya,

Njia hii ya kufunga mdomo wakati wa kukohoa au kupiga chafya huweza kusaidia kupunguza hatari ya kusambaza magonjwa ya kupumua, hivo hii pia ni mojawapo ya Njia za kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya kupumua.

– Punguza close contact na watu wote wenye dalili za magonjwa ya Kupumua,

dalili hizo ni pamoja na Kukohoa mara kwa mara,Kupiga chafya n.k.

– Nawa Mikono kwa maji Safi na Sabuni mara kwa mara

Moja ya njia muhimu sana ya kupunguza hatari ya kupata Magonjwa ya Kupumua ni pamoja na kunawa mikono kwa maji safi na Sabuni kila mara, kabla na baada ya kushika vitu mbali mbali,

Pia unaweza kutumia vitakasa Mikono maarufu kama Sanitizer

Hii pia ni mojawapo ya Njia za kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya kupumua.

– Hakikisha Usafi kila Mara,

Hapa tunazungumzia Usafi binafsi wa mwili,vyombo vya chakula, taulo za Kuogea n.k

– Epuka Kushirikiana na mtu mwingine vitu kama vile Taulo za kuogea,Mswaki,Mashuka n.k,

hasa kwa mtu mwenye dalili za magonjwa ya Kupumua.

– Pata Chanjo,

Njia za kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya kupumua ni Pamoja na kuchoma chanjo kwa yale magonjwa yote ya kupumua ambayo huweza kuzuilika kwa Njia ya chanjo.

– Waone wataalam wa afya kwa ajili ya Vipimo Zaidi,kama unapata dalili kama hizi;

  • Kukohoa mara kwa mara
  • Kupiga chafya
  • Kuhisi hali ya vidonda kooni
  • Homa
  • Kutoa sauti wakati wa kupumua
  • Kupata shida ya kupumua
  • Kutokwa na jasho hasa usiku
  • Kupata maumivu ya kifua wakati wa kupumua n.k

FAQs: Maswali ambayo huulizwa Mara kwa Mara

Je, magonjwa ya kupumua ni kama yapi?

Magonjwa ya kupumua ni kama vile;

✓ Ugonjwa wa pneumonia

✓ Ugonjwa wa Asthma.

✓ Tatizo la pneumothorax au atelectasis

✓ Tatizo la bronchitis

✓ chronic obstructive pulmonary disease (COPD)

✓ Saratani ya Mapafu(Lung cancer)

✓ Tuberculosis(TB)

✓ Tatizo la pulmonary edema n.k

Hitimisho

Yapo magonjwa ya Kupumua ambayo kwa kiasi kikubwa huhusisha mapafu pamoja na mfumo wa hewa kwa ujumla(respiratory diseases),

Njia za kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya kupumua kama vile pneumonia ni pamoja na;

Kuepuka kukaa kwenye maeneo ya Msongamano wa watu wengi,Kufunga mdomo wakati wa kukohoa au kupiga chafya,Kupunguza close contact na watu wote wenye dalili za magonjwa ya Kupumua,Kunawa Mikono kwa maji Safi na Sabuni mara kwa mara, kuhakikisha Usafi binafsi wa mwili,vyombo vya chakula, taulo za Kuogea n.k

-Kuepuka Kushirikiana na mtu mwingine vitu kama vile Taulo za kuogea,Mswaki,Mashuka n.k,hasa kwa mtu mwenye dalili za magonjwa ya Kupumua, Kupata Chanjo n.k

Pia hakikisha unafanya Vipimo pale tu unapoona dalili kama vile;

  • Kukohoa mara kwa mara
  • Kupiga chafya
  • Kuhisi hali ya vidonda kooni
  • Homa
  • Kutoa sauti wakati wa kupumua
  • Kupata shida ya kupumua
  • Kutokwa na jasho hasa usiku
  • Kupata maumivu ya kifua wakati wa kupumua n.k

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.