Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Ugonjwa wa manjano kwa watoto:chanzo,dalili na Tiba

Ugonjwa wa manjano kwa watoto:chanzo,dalili na Tiba

Ugonjwa wa manjano kwa watoto(Infant jaundice) ni hali ya mtoto kuwa na rangi ya manjano kwenye ngozi yake ya mwili Pamoja na machoni,

Na hali hii ya manjano kwa watoto hutokana na Damu ya Mtoto kuwa na kiwango kikubwa zaidi cha bilirubin, ambapo hii ni pigment ya njano kwenye seli nyekundu za damu.

Ugonjwa wa manjano kwa watoto hutokea sana kwa wale watoto waliozaliwa mapema yaani kabla ya wiki 37 za Ujauzito(watoto njiti/premature), na kwa baadhi ya watoto wanaonyonya bado,

Na hali hii ya manjano kwa watoto hutokea kwa Sababu Ini la mtoto bado halijakomaa vyakutosha ili kupambana na pigment ya bilirubin kwenye damu.

Dalili za Ugonjwa wa manjano kwa watoto

Dalili kubwa za Ugonjwa wa manjano kwa watoto ni Pamoja na;

  •  Ngozi ya Mtoto kuwa manjano
  •  Pamoja na Rangi ya macho kuwa manjano pia

Pia Kuangalia kama kuna Ugonjwa wa manjano kwa watoto, unaweza kubonyeza taratibu sehemu ya mbele ya kichwa cha mtoto au kwenye Pua,

Kama Ngozi ya maeneo haya ikionekana na rangi ya manjano sehemu ambapo umebonyeza basi tayari inaweza kuwa kiashiria mtoto wako ana Ugonjwa wa manjano kwa watoto(mild jaundice)

Hakikisha tu zoezi hili linafanyika kwenye Sehemu yenye mwanga mzuri au wakutosha na iwe mchana ni vizuri zaidi.

Chanzo cha Ugonjwa wa manjano kwa watoto

chanzo kikubwa cha Ugonjwa wa manjano kwa watoto ni uwepo wa kiwango kikubwa Zaidi cha bilirubin yaani kwa kitaalam hujulikana kama hyperbilirubinemia,

Bilirubin ni pigment inayosababisha rangi ya manjano kwa Watoto wenye shida hii.

Na kama nilivyosema hapo awali hali hii ya manjano kwa watoto hutokea kwa Sababu Ini la mtoto bado halijakomaa vyakutosha ili kupambana na pigment ya bilirubin kwenye damu.

Watoto wadogo huzalisha kiwango kikubwa cha bilirubin kuliko watu wazima, na hii ni kwasababu ya kuzalisha seli nyekundu za damu kwa kiwango kikubwa na kuzivunja kwa haraka sana ndani ya siku chache,

Kwa hali ya kawaida Ini hufanya kazi ya kuzichuja hizi bilirubin kutoka kwenye damu kisha kuziingiza kwenye utumbo,

Lakini kwa vile Ini la Mtoto bado halijakomaa vyakutosha haliwezi kuondoa kwa haraka kiwango cha kutosha cha bilirubin kwenye damu, Hali hii hupelekea uwepo wa kiwango kikubwa zaidi cha bilirubin.

Sababu Zingine ambazo huweza kuongeza hatari ya Ugonjwa wa manjano kwa watoto ni Pamoja na;

– Mtoto kupata tatizo la damu kuvuja kwa ndani yaani Internal bleeding (hemorrhage)

– Maambukizi kwenye damu ya mtoto (sepsis)

– Kuwa na tatizo kwenye Ini

– Mtoto kuzaliwa mapema au kabla ya wakati(Mtoto njiti/Premature)

– Watoto kutokunyonya vyakutosha,hali ambayo hupelekea kukosa virutubisho muhimu sana kwa mtoto

– Kuwa na tatizo kwenye Seli nyekundu za damu, hali ambayo hupelekea seli hizi kuvunjwa kwa haraka zaidi N.k

Kumbuka: Moja ya njia ya kuzuia uwepo wa Ugonjwa wa manjano kwa watoto ni kuhakikisha Mtoto wako ananyonya Vizuri na vyakutosha.

FAQs

1. Je Ugonjwa wa manjano kwa watoto unasababishwa na nini?

chanzo kikubwa cha Ugonjwa wa manjano kwa watoto ni uwepo wa kiwango kikubwa Zaidi cha bilirubin yaani kwa kitaalam hujulikana kama hyperbilirubinemia,

Bilirubin ni pigment inayosababisha rangi ya manjano kwa Watoto wenye shida hii.

2. Je ni kundi lipi la watoto ambao wapo kwenye hatari zaidi ya Kupata Ugonjwa wa manjano kwa watoto?

– Watoto ambao huzaliwa mapema au kabla ya wakati(Mtoto njiti/Premature)

– Watoto ambao hawanyonyi vyakutosha,hali ambayo hupelekea kukosa virutubisho muhimu sana kwa mtoto

– Watoto wenye tatizo kwenye Seli nyekundu za damu, hali ambayo hupelekea seli hizi kuvunjwa kwa haraka zaidi.

Hitimisho:

Ugonjwa wa manjano kwa Watoto hutokea kwa watoto wengi ila kwa bahati nzuri unaweza Kutibika na mtoto kurudi kwenye hali yake ya kawaida,

chanzo kikubwa cha Ugonjwa wa manjano kwa watoto ni uwepo wa kiwango kikubwa Zaidi cha bilirubin yaani kwa kitaalam hujulikana kama hyperbilirubinemia,

Sababu Zingine ambazo huweza kuongeza hatari ya Ugonjwa wa manjano kwa watoto ni Pamoja na;Mtoto kupata tatizo la damu kuvuja kwa ndani yaani Internal bleeding (hemorrhage),

Maambukizi kwenye damu ya mtoto (sepsis), Kuwa na tatizo kwenye Ini, Mtoto kuzaliwa mapema au kabla ya wakati(Mtoto njiti/Premature),Watoto kutokunyonya vyakutosha,hali ambayo hupelekea kukosa virutubisho muhimu sana kwa mtoto,kuwa na tatizo kwenye Seli nyekundu za damu, hali ambayo hupelekea seli hizi kuvunjwa kwa haraka zaidi N.k

Kumbuka: Moja ya njia ya kuzuia uwepo wa Ugonjwa wa manjano kwa watoto ni kuhakikisha Mtoto wako ananyonya Vizuri na vyakutosha.

Ukiona dalili zozote za Ugonjwa wa manjano kwa watoto hakikisha unampeleka mtoto wako hospital mapema kwa ajili ya Msaada Zaidi.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.