Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Magonjwa ya jicho,Soma hapa magonjwa mbali mbali ya macho

Magonjwa ya jicho,Soma hapa magonjwa mbali mbali ya macho

Katika Makala hii tumeelezea Magonjwa ya jicho ambayo hutokea mara kwa mara kwa watu wengi Zaidi,Soma hapa kufahamu.

Magonjwa ya jicho

Hii hapa ni orodha ya magonjwa mbali mbali ya macho;

1. Refractive Errors, Tatizo hili huhusisha zaidi kuathiriwa uwezo wa macho kuona, kama vile; Macho kutokuona mbali,macho kutokuona karibu au macho kutokuona mbali wala karibu,

ambapo hapa tuna aina mbali mbali ikiwemo;

2. Age-Related Macular Degeneration

Tatizo hili ni miongoni mwa Magonjwa ya jicho ambayo hutokea kutokana na mtu kuwa mzee(umri mkubwa), hali ambayo huathiri uwezo wa jicho au macho kuona.

3. Tatizo la Mtoto wa jicho(Cataract)

Cataract huhusisha uwepo wa wingu kwenye lensi ya macho kisha kusababisha macho kuona kitu kama wingu mbele,

Mtoto wa jicho(cataract) ni miongoni mwa Magonjwa ya jicho ambayo huongoza kwa kusababisha tatizo la upofu duniani kote.

4. Tatizo la Diabetic Retinopathy

Hii ni miongoni mwa Magonjwa ya jicho ambayo hutokana na athari za Ugonjwa wa Kisukari,

Diabetic retinopathy (DR) pia ni miongoni mwa Magonjwa ya jicho ambayo husababisha wagonjwa wengi wa Sukari kuwa na tatizo ya macho kutokuona.

5. Tatizo la Presha ya Macho(Glaucoma)

Presha ya macho ni miongoni mwa Magonjwa ya jicho ambayo huwapata watu wengi na kusababisha tatizo la macho kutokuona,

Presha ya macho(Glaucoma) ni kundi la magonjwa ambayo yanaweza kuharibu mishipa ya macho au eye’s optic nerve na kusababisha uwezo wa macho kuona kupotea na kuleta upofu wa macho.

Glaucoma hutokea wakati shinikizo la kawaida la maji ndani ya macho linapanda polepole.

6. Tatizo la Amblyopia au “lazy eye,”

Tatizo hili ni miongoni mwa Magonjwa ya jicho ambayo husababisha shida ya macho kutokuona hasa kwa Watoto,

Tatizo hili hutokea pale ambapo uwezo wa jicho moja kuona hupungua zaidi,KwaSababu jicho na ubongo havifanyi kazi vizuri kwa pamoja.

Hapa Jicho huonekana lipo kawaida bila shida yoyote lakini halioni vizuri, kwa Sababu Ubongo unapendelea jicho lingine Zaidi.

7. Tatizo la Strabismus
Strabismus ni miongoni mwa Magonjwa ya jicho ambayo huhusisha kukosa uwiano(imbalance) katika nafasi ya macho mawili.

Strabismus inaweza kusababisha macho kuvuka kwa kuingia ndani (esotropia) au kugeuka nje (exotropia). Strabismus husababishwa na ukosefu wa uratibu kati ya macho,

Matokeo yake, macho hutazama kwa njia au muelekeo(direction) tofauti na hayawezi kutazama eneo moja kwa wakati mmoja

Au tunasema” As a result, the eyes look in different directions and do not focus simultaneously on a single point”.

Katika hali nyingi za strabismus kwa watoto, sababu haijulikani.

Hitimisho

Yapi magonjwa mbali mbali ambayo huweza kuathiri  macho yako,Hii hapa ni orodha ya Magonjwa ya jicho ambayo huwapata watu wengi zaidi;

Ugonjwa wa presha ya macho(Glaucoma),Tatizo la Mtoto wa jicho(cataract),Refractive Errors ambapo hapa tuna aina mbali mbali ikiwemo;

Age-Related Macular Degeneration,Tatizo la Diabetic Retinopathy,Tatizo la Amblyopia au “lazy eye,”Tatizo la Strabismus n.k

 

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.