Tatizo la maumivu ya korodani,chanzo,dalili na Tiba
Tatizo la maumivu ya korodani,chanzo,dalili na Tiba
Katika Makala hii tumechambua Zaidi kuhusu chanzio cha Tatizo la Maumivu ya Korodani,tatizo ambalo huweza kumpata Mwanaume yoyote.
Tatizo la maumivu ya korodani
Tatizo la maumivu ya korodani linaweza kuwa la muda mfupi(acute) au likawa tatizo endelevu(chronic), hii ni kulingana na chanzo husika cha tatizo hili,
Na hapa tumeelezea Sababu mbali mbali za Tatizo la maumivu ya korodani
Chanzo cha Tatizo la maumivu ya korodani
Zipo Sababu mbali mbali ambazo huweza kupelekea mtu kupata Tatizo la maumivu ya korodani ikiwemo;
1. Kuharibiwa kwa Nerves kutokana na magonjwa mbali mbali kama vile Ugonjwa wa Kisukari(Diabetic neuropathy)
2. Mtu kupata ajali au Kuumia(Trauma/ injury) eneo la Korodani, Hii pia huweza kusababisha Tatizo la maumivu ya korodani
3. Kupata tatizo la Uvimbe kwenye Korodani, tatizo la Epididymitis n.k
4. Kupata tatizo la Busha au Hydrocele, tatizo la maji kujaa na kusababisha kuvimba kwa korodani
5. Kupata tatizo la Hernia hasa aina hii ya Inguinal hernia
6. Kupata tatizo la Mawe kwenye figo yaani Kidney stones, Hata hii pia huweza kusababisha Tatizo la maumivu ya korodani
7. Kupata tatizo la maambukizi au Kuvimba kwa tezi dume(Prostatitis)
8. Kupata maambukizi ya magonjwa mbali mbali kama vile UTI n.k,
maambukizi haya ya magonjwa huweza kupelekea mtu kupata Tatizo la maumivu ya korodani
9. Kupata tatizo la Testicular torsion (twisted testicle)
10. Kupata tatizo la kuvimba au kupanuka kwa mishipa ya veins ndani ya Korodani(Varicocele),
vyote hivi huweza kupelekea mtu kupata Tatizo la maumivu ya korodani
11. Pia Tatizo la maumivu ya korodani huweza kusababishwa na magonjwa mbali mbali ya Zinaa(Sexual transmitted diseases-STD’s) kama vile;Ugonjwa wa chlamydia
12. Tatizo la gangrene, ambapo tissue mbali mbali za mwili hufa, kutokana na Sababu mbali mbali ikiwemo;
- kuumia,
- magonjwa kama KiSukari,
- tatizo la testicular torsion ambalo halikutibiwa n.k
FAQs: Maswali ambayo huulizwa mara kwa mara
Je,Uvimbe kwenye Korodani huweza kusababisha Tatizo la maumivu ya korodani?
Ndyo,Moja ya Sababu za mtu kupata Tatizo la maumivu ya korodani ni pamoja na kuwa na Uvimbe ndani ya Korodani,kuvimba kwa vimishipa vidogo kwenye eneo hili n.k
Hitimisho
Tatizo la maumivu ya korodani ni tatizo ambalo huweza kumpata Mwanaume yoyote,
Zipo Sababu mbali mbali zinazopelekea mtu kupata Tatizo la maumivu ya korodani,sababu hizo ni pamoja na;
Mtu kuumia eneo la korodani,kuharibiwa kwa nerves kutokana na magonjwa mbali mbali kama vile Kisukari, kuwa na Uvimbe kwenye korodani,maambukizi ya magonjwa ya Zinaa kama vile chlamydia,
Mwanaume kupata tatizo la kutanuka kwa mishipa ya Veins kwenye korodani kwa kitaalam hujulikana kama “Varicocele”, kupata maambukizi au Kuvimba kwa Tezi Dume n.k
Ukiona unapata Tatizo la maumivu ya korodani,hakikisha unaongea na wataalam wa afya ili kujua chanzo ni nini,na kisha kupata msaada wa matibabu mapema.
KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.
Dr.uko vizuri sana mkuu nafikiri wanaweza kuwa msaada mkubwa sana
Oh, asante sana rafk 🙏🙏