Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

kulala kwa dakika 30 kwa siku kwa muda wa mchana kunaweza kuchangia kupunguza kasi ya kusinyaa kwa ubongo

kulala kwa dakika 30 kwa siku kwa muda wa mchana kunaweza kuchangia kupunguza kasi ya kusinyaa kwa ubongo.

Utafiti mpya kutoka Chuo cha UCL na Chuo Kikuu cha Jamhuri nchini Uruguay unaonesha kuwa kulala mara kwa mara wakati wa mchana kunaweza kuimarisha afya ya ubongo kutokana na kupunguza kasi ya akili kusinyaa au kupunguza uwezo wa kufanya kazi pindi umri unavyozidi kusogea.

Wanasayansi wamependekeza kwamba kulala kwa dakika 30 kwa siku kwa muda wa mchana kunaweza kuchangia kupunguza kasi ya kusinyaa kwa ubongo.

Utafiti huo uliochapishwa katika jarida la afya ya usingizi umefanywa baada ya kukusanya taarifa kutoka kwa Watu 378,932 kutoka kwenye “Biobank” ya kuhifadhia taarifa za raia ya nchini Uingereza.

Utafiti huo umeonesha Watu waliolala mchana hali ya afya ya ubongo wao ilikuwa vizuri zaidi kuliko wasiokuwa na tabia ya kulala huku ukieleza kuwa usingizi una faida kubwa ya kuepusha changamoto za afya ya akili.
Via: MillardAyoUPDATES

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.