Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Magonjwa mengi yanasababishwa na mitindo ya kisasa ya maisha

Magonjwa mengi yanasababishwa na mitindo ya kisasa ya maisha

Fahamu kwamba,Asilimia kubwa ya magonjwa haya ni magonjwa yasioyakuambukiza(non-communicable diseases) ambayo hutokana na mtindo mbaya wa maisha(bad lifestyle),

Aina mbali mbali ya Magonjwa yatokanayo na Mtindo wa Maisha

Haya hapa ni Magonjwa mbali mbali kutokana na Mtindo wa Maisha;

1. Magonjwa ya Moyo(Heart Diseases)

Magonjwa ya moyo ni mfano wa magonjwa yanayotokana na mtindo wa maisha na huhusisha matatizo kwenye moyo, vali zake, misuli, mishipa, au njia za ndani za umeme zinazohusika na kusinyaa kwa misuli.

Baadhi ya matatizo ya moyo ni pamoja na:

  • Heart failure
  • Arrhythmias
  • Cardiomyopathy
  • Coronary artery disease
  • Heart valve disease

Sabavu hizi huongeza hatari ya Mtu kupata magonjwa mbali mbali ya Moyo;

✓ Umri mkubwa

✓ Uvutaji wa Sigara

✓ Ulaji Mbaya(Poor diet)

✓ Tatizo la Presha ya kupanda(High blood pressure)

✓ ugonjwa wa Kisukari

✓ kuwa na kiwango kikubwa cha cholesterol kwenye damu

✓ Uzito kupita kiasi pamoja na Unene(Overweght/Obesity)

✓ Kutofanya Mazoezi

✓ kuwa Na Msongo mkali wa mawazo/Stress n.k

Vipimo ambavyo huweza kufanyika

  • Coronary angiography
  • CT scans
  • Radionuclide tests
  • MRI scans
  • Echocardiogram
  • Blood tests
  • X-rays
  • Electrocardiogram (ECG)
  • Exercise stress tests

2. Tatizo la Uzito mkubwa pamoja na Unene(Overweight/Obesity)

Watu huweza kuwa na Uzito mkubwa kupita kiasi na wanene kwa sababu ya ulaji mbaya, kupungua kwa shughuli za mwili ikiwemo kutokufanya Mazoezi, maisha ya msongo wa mawazo kila mara, na mambo mengine.

3. Ugonjwa wa Kisukari(Type 2 Diabetes)

Aina ya 2 ya kisukari huhusisha hali ambapo seli haziwezi kutumia glucose au sukari kwenye damu kwa ufanisi kwa ajili ya nishati. Hii hutokea wakati seli zinapokuwa Insensitive kwa insulini, na viwango vya sukari kwenye damu hatua kwa hatua huwa juu sana.

Mchanganyiko wa mambo kadhaa kama vile seli za beta zilizovunjika, uzito mkubwa, ugonjwa wa kimetaboliki, n.k., huwajibika kuwa miongoni mwa sababu ya ugonjwa huu.

Vitu hivi huweza kuongeza hatari ya Mtu kupata Ugonjwa wa Kisukari Aina ya Pili

  • Kuwa na Uzito Mkubwa kupita kiasi
  • Kunywa Sana Soda,Pombe n.k
  • Matumizi ya Sukari Kupita kiasi
  • Kula vyakula vya Kusindika(processed food) Pamoja na vyakula vyenye simple carbohydrates
  • Sababu za kigenetics au kuwa na watu wenye Ugonjwa wa Kisukari kwenye Familia yako
  • Kutokufanya Mazoezi ya mwili n.k

4. Ugonjwa wa kiharusi au Stroke
Zipo Sababu mbali mbali ambazo huweza kuongeza hatari ya mtu kupata Ugonjwa wa Kiharusi ikiwemo;

  • Kuwa na tatizo la Presha ya kupanda(High blood pressure)
  • Kuwa na Ugonjwa wa Kisukari
  • Kuwa na kiwango kikubwa cha cholesterol kwenye damu
  • Uvutaji wa Sigara
  • Kuwa na matatizo ya moyo kama vile heart rhythm disturbances au atrial fibrillation

Vipimo ambavyo huweza Kufanyika

✓ Kipimo cha damu(Blood tests)

✓ Carotid ultrasound

✓ Computerized tomography (CT) scan

✓ Physical exams

✓ Magnetic resonance imaging (MRI)

✓ Echocardiogram

✓ Cerebral angiogram

5. Ugonjwa wa shinikizo la juu la damu(high blood pressure)

Sababu hizi huweza kuongeza hatari ya mtu kupata Ugonjwa wa Presha

  • Family history
  • Kuwa na Uzito mkubwa au unene(Overweight/Obesity)
  • Umri mkubwa
  • Kutokufanya mazoezi
  • Matumizi ya tumbaku
  • Unywaji wa Pombe kupita kiasi
  • Matumizi ya chumvi kupita kiasi
  • Kuwa na magonjwa mengine kama vile; Ugonjwa wa figo,Ugonjwa wa kisukari n.k

6. Kuwa na magonjwa ya Mapafu kama vile Chronic Obstructive Pulmonary Diseases (COPD)

Ambapo huweza kutokana na Uvutaji wa Sigara,Sababu za kimazingira kama vile uchafuzi wa hewa, gases leaks n.k

Vipimo ambavyo huweza kufanyika ni Pamoja na;

✓ Chest X-ray

✓ Lung (pulmonary) function tests

✓ Laboratory tests

✓ Arterial blood gas analysis

✓ CT scan n.k

7. Ugonjwa wa Pumu au Asthma

Pumu(Asthma) huweza kusababishwa na kupungua au uvimbe wa njia za hewa. Ugonjwa huu husababisha mtu kupata shida ya kupumua,kukohoa kwa muda mrefu,kifua kubana n.k.

Ingawa chanzo halisi cha pumu hakijulikani, watu lazima watambue sababu mbalimbali za hatari zinazoweza kuongeza uwezekano wa kupata pumu. Hizi zimeorodheshwa kama ifuatavyo:

  • Kuwa na uzito kupita kiasi
  • Kuwa na ndugu wa damu (mzazi au ndugu) mwenye pumu
  • Kuvuta sigara
  • Kuwa na hali nyingine ya mzio au allergies kama vile atopic dermatitis
  • uchafuzi wa mazingira
  • kemikali zinazotumika katika utengenezaji wa vitu viwandani, utengenezaji wa nywele na kilimo
  • Kukabiliwa na moshi wa sigara n.k

8. Tatizo la Osteoporosis

Sababu hizi huongeza hatari ya Mtu kupata tatizo hili la Mifupa;

– Upungufu wa Vitamin D

– Uvutaji wa Sigara

– Kula mlo wenye kiwango kidogo sana cha calcium

– Family history ya osteoporosis

– Kuwa na magonjwa mengine kama vile chronic hepatitis C, rheumatoid arthritis n.k

– Kutokufanya mazoezi

– Matumizi ya caffeine kupita kiasi

– Unywaji wa Pombe kupita kiasi

– Pia tatizo kama vile Hyperthyroidism pamoja na hyperparathyroidism huweza kuhusika.n.k

Mwisho, Zingatia Mambo haya ili Kujikinga na Magonjwa yanayotokana na mtindo mbaya wa Maisha;

  1. Kula Mlo Kamili(balance diet)
  2. Hakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku
  3. Fany Mazoezi ya mwili angalau kwa dakika 30 kila siku
  4. Dhibiti Uzito wako wa mwili na kuhakikisha unaepuka tatizo la Uzito kupita kiasi pamoja na Unene
  5. Epuka Uvutaji wa Sigara
  6. Epuka matumizi ya Pombe kupita kiasi
  7. Epuka matumizi ya chumvi nyingi au Sukari nyingi
  8. Epuka matumizi ya Caffeine kwa kiwango kikubwa sana
  9. Epuka ulaji wa vyakula vya mafuta mengi sana
  10. Onana na Wataalam wa afya kama unahisi dalili zozote za magonjwa

AU KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO LOLOTE TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.