Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Hadi kufikia tarehe 31 Mei, 2023 jumla ya watu waliopata maambukizi ya ugonjwa wa Marburg walikuwa watu tisa (9)

Hadi kufikia tarehe 31 Mei, 2023 jumla ya watu waliopata maambukizi ya ugonjwa wa Marburg walikuwa watu tisa (9)

“Hadi kufikia tarehe 31 Mei, 2023 jumla ya watu waliopata maambukizi ya ugonjwa wa Marburg walikuwa watu tisa (9),

kati ya hao wagonjwa watatu (3) wamepona akiwemo daktari wa kituo cha Afya Maruku aliyewahudumia wagonjwa wa mwanzo.

Aidha, wagonjwa sita (6) walipoteza maisha akiwemo mtaalamu wa maabara kutoka Kituo cha Afya Maruku na mtoto mwenye umri wa miezi 18 ambaye mama yake ni miongoni mwa wagonjwa waliopona.

Miongoni mwa waliofariki watu watano (5) walikuwa ndugu wa ukoo na mmoja alikuwa mtumishi wa kituo cha afya Maruku. Mgonjwa wa mwisho alibainika kuwa hana maambukizi (Negative) tarehe 19 Aprili 2023”

Amesema Mganga Mkuu wa Serikali Prof Tumaini Nagu akiwasilisha taarifa ya kitaalam ya kukabiliana na Ugonjwa wa Marburg kwenye Kilele cha Mapambano dhidi ya ugonjwa huo nchini Tanzania.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.