Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Muda unaofaa kufua TAULO ni angalau mara moja kwa wiki

Kwa kunusa tu Taulo yako au kuichunguza kwa uangalifu ikiwa haina mabaka, tunaweza kuamua ikiwa iko tayari kufuliwa au inaweza kustahimili matumizi mengine.

Lakini tunajuaje ni wakati wa kufua taulo? Je, ni mara ngapi tunapaswa kufua kipande hiki cha kitambaa tunachotumia kukausha miili yetu baada ya kuoga?

Uchunguzi wa hivi karibuni huko Uingereza wa watu 2,200, uligundua kuwa watu wengi hawana uhakika. 44% walionyesha kuwa wanafua taulo kila baada ya miezi mitatu au zaidi. Mtu mmoja kati ya watano walisema hufua mara moja kwa mwezi, 25% mara moja kwa wiki, na mmoja kati ya 20 hufua kila baada ya kuoga.

Kwa nini unapaswa kufua taulo?

BBC ilimuuliza Dkt. Sally Bloomfield, mtaalamu wa usafi na uzuiaji wa magonjwa ya kuambukiza, anasema “muda unaofaa ni angalau mara moja kwa wiki. Ingawa taulo inaweza kuonekana ni safi, ila imekusanya mamilioni ya bakteria na wanaweza kuwa hatari kwa afya.”

Ikiwa hutafua mara kwa mara, anasema mtaalamu huyo, “idadi ya bakteria kwenye taulo huongezeka, na unapoamua kufua ni vigumu sana kuwaondoa wote.”

Tunapokausha sehemu tofauti za mwili wetu, taulo hupata bakteria. Bakteria wengi wanaoishi kwenye ngozi zetu wanaweza kuwa wasiwe wa kuambukiza, lakini ikiwa wataingia kupitia vidonda au kupenya kwenye ngozi wanaweza kusababisha maambukizi,” Bloombield anasema.

Je, ikiwa unaishi peke yako?

Ikiwa unaishi na watu wengine, unapaswa kuwa mwangalifu zaidi.

“Wakati mwingine, tunaweza kuwa na bakteria ambao hawasababishi magonjwa kwetu, lakini tukiwapitisha kwa watu mwingine, wanaweza kuleta magonjwa,” anasema mtaalamu.

“Bakteria wanaweza kusafirishwa ikiwa mtu mwingine atatumia taulo hiyo au ikiwa utaiosha na nguo nyingine,” anaongeza.

Unaweza kufikiria kuwa ikiwa unaishi peke yako, hatari ni ndogo. Na ni kweli, lakini, Bloomfield anashauri – hata katika hali hiyo, “hupaswi kuruhusu zaidi ya siku 15 kupita bila ya kuiosha.”

Cristina Psomadakis, daktari wa ngozi katika Shirika la Taifa la Afya nchini Uingereza (NHS), anawahimiza watu kuchunguza ni mara ngapi wanafua taulo zao.

“Ikiwa wewe ni mtu ambaye una chunusi usoni au mwilini, unapaswa uoshe taulo yako mara kwa mara. Lazima ushughulikie usafi wako, au mambo yataendelea kuharibika.”

Usafi duni nyumbani – ikiwa ni pamoja na taulo – unaweza kuwa sababu ya kuchangia matatizo ya ngozi.

Taulo mbili tofauti

Ikiwa unafanya mazoezi, huenda una kitambaa cha kufutia jasho. Ikiwa unatumia taulo katika matukio kama hayo, Bloomfield anasema unahitaji kuiosha mara kwa mara.

“Unaongeza jasho, na unaondoa seli za juu ya ngozi ya mwili wako, na bakteria zaidi huishia kwenye taulo.”

Usipoiosha mara kwa mara, anasema, “itachafuka sana na itakuwa vigumu zaidi kuisafisha siku utakapo amua kuiosha.”

Na ikiwa unajiuliza; je unahitaji taulo moja kwa ajili ya mwili wako na moja kwa ajili ya uso wako, Psomadakis anapendeza ndio zinapaswa kuwa taulo mbili tofauti.

“Usisahau kwamba unapotumia taulo ya mwili, unakaushia mahali ambapo jua halifiki, unaweza kuwa na aina fulani ya bakteria ambao hutaki wafike kwenye uso wako,” anasema.

Bloomfield anakubali kuwa kuna wasiwasi kuhusu mazingira na gharama ya kutumia mashine za kuoshea, lakini anasema ni bora kuiosha mara kwa mara kwa kwa joto la wastani kuliko kuiosha kwa joto la juu baada ya kipindi kirefu.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.