Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Siku ya Mtoto wa Afrika,kuelekea Juni 16,2023

Siku ya Mtoto wa Afrika,kuelekea Juni 16,2023

Maadhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika ambayo yatafanyika tarehe 16,Juni 2023

KauliMbiu:

“Zingatia Usalama wa Mtoto katika Ulimwengu wa kidijitali”

Bado siku 3.!!

Tarehe 16 Juni kila Mwaka Jumuiya ya Kimataifa inaadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika ULIMWENGU

Kunako Mwaka 1991, Wakuu wa OAU walianzisha Siku ya Mtoto wa Afrika kama kumbukumbu ya uasi dhidi ya wanafunzi uliotokea hapo tarehe 16 Juni 1976 huko Soweto, Afrika Kusini.

Wakati huo, wanafunzi waliandamana, mosi kupinga mfumo na elimu duni waliokuwa wanapatiwa. Pili, waliitaka Serikali ya kibaguzi ya Afrika ya Kusini kuboresha mfumo wa lugha ya kufundishia.

Siku ya Mtoto wa Afrika hutumika kuwakumbusha watoto wetu hatua ya kijasiri waliyoichukua wenzao huko Afrika Kusini katika kulinda utu, heshima na haki zao msingi.

Watoto wanakumbushwa kwamba wanaweza kuleta mabadiliko hata wakiwa wadogo,

Hii ni Siku ya Kimataifa inayopania kuboresha hali na mazingira ya elimu kwa watoto Barani Afrika.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.