Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Tatizo la Macho kutokuona mbali,chanzo,dalili na Tiba yake

Tatizo la Macho kutokuona mbali,chanzo,dalili na Tiba yake

Tatizo la macho kutokuona mbali ni tatizo ambalo kwa kitaalam hujulikana kama Nearsightedness (myopia), tatizo hili huhusisha mtu kuona vitu vilivyo karibu,vitu hivi vilivyo karibu huonekana vizuri kwa uwazi, lakini vitu vilivyo mbali zaidi vinaonekana kuwa na ukungu.

Tatizo la macho kutokuona mbali kwa kawaida hutokea wakati wa utoto na ujana, na kwa kawaida huonekana zaidi mtu akiwa na umri kati ya miaka 20 na 40, Tatizo hili la Myopia huwa ndani ya familia husika.

Dalili za Tatizo la Macho kutokuona mbali

Dalili za Tatizo la Macho kutokuona mbali ni Pamoja na;

– Uoni hafifu unapotazama vitu vilivyo mbali

– Kupepesa macho au kufunga kope kwa kiasi ili kuona vizuri

– Maumivu ya kichwa

– kuwa na tatizo la Mkazo wa macho

– Watoto wanaweza kupata shida ya kuona vitu kwenye ubao mweupe au kwenye projector wakiwa darasani.

– Watoto wadogo wanaweza wasionyeshe dalili za tatizo la Macho kutokuona mbali, lakini wanaweza kuwa na tabia zifuatazo;

  • Kutotambua vitu vilivyo mbali
  • kupepesa macho kupita kiasi
  • Kusugua macho mara kwa mara

– Watu wazima walio na tatizo la Macho kutokuona mbali wanaweza kupata shida ya kusoma alama za barabarani. Watu wengine wanaweza kuona giza kwenye mwanga hafifu, kama vile kuendesha gari wakati wa usiku, hata kama wanaona vizuri mchana. Hali hii kwa kitaalamu inaitwa night myopia.

Chanzo cha Tatizo la Macho kutokuona mbali

Jicho lako lina sehemu mbili zinazolenga picha:

  1. Konea(cornea)
  2. lenzi(lens)

Ili uweze kuona, mwanga lazima upite kwenye konea na lenzi. Hizi ndiyo zinakunja (refract) mwanga, ili mwanga uelekezwe moja kwa moja kwenye tishu za neva (retina) nyuma ya jicho lako. Tishu hizi hutafsiri mwanga katika ishara zinazotumwa kwenye ubongo, ambapo hukuwezesha kutambua picha.

Sasa basi,tatizo la Macho kutokuona mbali hutokea pale ambapo kuna shida kwenye Mwanga kujikunja au kwa kitaalamu Refractive errors,

Tatizo hili hutokea wakati sura au hali ya cornea – au sura ya jicho yenyewe – husababisha Mwanga kulenga vibaya wakati unapita kwenye jicho.

Tatizo la Macho kutokuona mbali kwa kawaida huweza kutokana na jicho kuwa na umbo la mviringo(oval-shaped) badala ya duara. Pia kutokana na mkunjo wa konea kuwa mwinuko sana.

Mabadiliko haya husababisha miale ya mwanga kufika mahali mbele ya retina na kuvuka. Ujumbe unaotumwa kutoka kwenye retina hadi kwenye ubongo unatafsiriwa kuwa kama ukungu.

Matibabu ya Tatizo la Macho kutokuona mbali

Tatizo hili la macho kutokuona mbali huweza kuhusisha matibabu ya aina mbalimbali ikiwemo;

  • Matumizi ya miwani sahihi kulingana na vipimo(corrective lenses)
  • Au huduma ya Upasuaji(refractive surgery).

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA JUU YA TATIZO HILI TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.