Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Avunja Record ya Dunia kwa kutoa Maziwa yake kwa maelfu ya watoto Njiti

Avunja Record ya Dunia kwa kutoa Maziwa yake kwa maelfu ya watoto Njiti:

Mwanamke mmoja amevunja record ya Dunia na kuandikwa kwenye jarida la Guiness World records” baada ya kuchangia maziwa yake kwa maelfu ya watoto ambao huzaliwa kabla ya wakati/watoto ambao huzaliwa mapema/watoto njiti(Premature babies).

Elisabeth Anderson-Sierra ni mama wa watoto wawili ambaye amelisha maelfu ya watoto – hata kusaidia kuokoa maisha ya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati,

Elisabeth Mzaliwa wa Aloha, Oregon, Marekani, aliweka rekodi ya mchango mkubwa zaidi wa maziwa ya mama kutoka kwa mtu mmoja,ambaye aliweza kuchangia lita 1,599.68 (56,301.20 UK fl oz) kwa benki ya maziwa kati ya tarehe 20 Februari 2015 na 20 Juni 2018,

Hiyo ni sawa na chupa 800 za lita 2 za Coke!

“Hii ni hesabu tu ya maziwa ambayo nilitoa kwa benki ya maziwa kati ya mwaka wa 2015 na 2018,” alisema Elisabeth.

“This only accounts for milk that I donated to a milk bank between the years of 2015 and 2018,” said Elisabeth. 

Katika kipindi cha miaka tisa iliyopita, Elisabeth ametoa mchango kwa familia za ndani na wapokeaji duniani kote na anakadiria jumla ya kiasi cha maziwa yaliyotolewa kuwa zaidi ya wakia 350,000(ounces).

Yeye hutoa maziwa yake na kuchangia kwa watoto wengi ambao wameitwa “watoto ambao wameshindwa kustawi.”

Elisabeth amesema lengo lake kubwa ni kuhakikisha anaondoa hilo jina ambalo watoto njiti au watoto ambao huzaliwa mapema/kabla ya wakati wamepewa.

Anasema; ““Haya ndiyo mambo ninayozingatia. Haya ndiyo mazuri na ndyo sababu kwa nini ninaendelea kufanya ninachofanya.”

“These are the things that I focus on. These are the positives and why I continue doing what I do.” 

Katika tukio moja, Elisabeth alikuwa Puerto Rico na mumewe baada ya Kimbunga Maria kupiga mnamo Septemba 2017.

“Mume wangu ni mwenyeji wa Puerto Rico na tulikuwa tumeenda Puerto Rico mara tu baada ya Kimbunga Maria,” alisema.

Juhudi zake za kuchangia maziwa kwa watoto njiti zilionekana hata kwenye Majanga mbali mbali ya Dunia,

Mchango wake mkubwa wa kutoa Maziwa yake kwa watoto ambao huzaliwa kabla ya wakati(watoto njiti-premature babies) ulionekana kisha kuweza kuvunja record ya Dunia.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.