Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
Magonjwa

Maumivu ya tumbo upande wa kushoto chanzo chake

Maumivu ya tumbo upande wa kushoto chanzo chake

Hizi hapa ni baadhi ya sababu zinazopelekea maumivu ya tumbo upande wa kushoto;

1. Ugonjwa wa UTI

Mtu mwenye Ugonjwa wa UTI huweza kupata shida ya maumivu ya tumbo hasa upande wa kushoto karibu na kitovu

2. Kuwa na tatizo la Diverticulitis

Mara nyingi, maumivu ya kudumu upande wa chini kushoto mwa tumbo husababishwa na tatizo la diverticulitis.

Diverticula ni vifuko vidogo vilivyoundwa kutokana na shinikizo kwenye maeneo dhaifu ndani ya utumbo mkubwa(Colon). Vifuko hivi(Diverticula) hutokea sana kwa watu wenye umri wa zaidi ya miaka 65. Wakati vifuko hivi vikichanika, kuvimba na kupata maambukizi vinaweza kusababisha tatizo linalojulikana kama diverticulitis.

Tatizo hili huambatana na dalili zingine kama vile;

  • Homa
  • Kichefuchefu au kutapika
  • Kuharisha au kupata choo kigumu
  • Maumivu ya tumbo n.k
  • fever

3. Tatizo la Gas

Kupitisha gesi ni mchakato wa kawaida kwenye mfumo wa umeng’enyaji chakula. Gesi hupatikana katika njia yako yote ya usagaji chakula, kuanzia tumboni hadi kwenye puru(rectum). Ila Gesi ikiwa nyingi inaweza kusababisha maumivu, uvimbe, na usumbufu kwako.

Gesi sio tatizo ambalo ni kubwa sana ila Ongea na daktari ikiwa inaendelea au inaambatana na dalili zingine, kama vile:

  • kutapika
  • kuharisha au kuvimbiwa
  • kupoteza uzito bila kukusudia
  • Kupata kiungulia kila mara
  • Kutoa damu kwenye kinyesi n.k

4. Tatizo la Indigestion

Indigestion ni tatizo ambalo huhusisha maumivu ya tumbo au Usumbufu wa sehemu ya juu ya tumbo unaoambatana na hali ya kuungua, kuvimbiwa au kuwa na gesi, kichefuchefu au kushiba haraka sana baada ya kuanza kula.

Indigestion kawaida hutokea baada ya kula. Tumbo lako hutengeneza asidi wakati unakula, ambayo inaweza kuwasha umio, tumbo, au utumbo. Maumivu huwa katika sehemu ya juu ya tumbo, lakini katika hali ambayo ni nadra sana, inaweza pia kuathiri sehemu ya chini ya tumbo.

Dalili kubwa za tatizo la indigestion ni pamoja na:

  • Kupata maumivu ya tumbo ikiwemo upande wa kushoto
  • Kupata kiungulia(heartburn)
  • Kuhisi hali ya kuungua tumboni(burning sensation)
  • Kuhisi umeshiba au kuvimbiwa
  • Kutoa gesi
  • Kuhisi kichefuchefu

5. Tatizo la Hernia

Hernia ni matokeo ya kiungo cha ndani kusukuma misuli au tishu zinazokizunguka. Hii inaweza kusababisha kutuna au uvimbe kutokea sehemu ya chini ya tumbo, kinena, au sehemu ya juu ya paja.

Dalili zingine zinaweza kujumuisha:

  • kuongezeka kwa ukubwa wa uvimbe
  • kuongezeka kwa maumivu kwenye eneo lilioathiriwa
  • maumivu wakati wa kuinua kitu
  • Kupata maumivu makali ya tumbo
  • kuhisi kushiba n.k

6. Tatizo la mawe kwenye Figo(Kidney stones)

Tatizo hili huweza kusababisha maumivu wakati mawe haya yanaposogea ndani ya figo yako au kwenye ureta, ambao ni mrija unaounganisha figo na kibofu.

Unaweza kupata maumivu makali upande mmoja wa tumbo au mgongo, chini ya mbavu zako. Hii inaweza kuja wakati jiwe linaposogea kwenye njia yako ya mkojo.

Unaweza pia kupata dalili zingine ikiwemo:

  • mkojo kuwa na rangi ya Pinki, nyekundu, hudhurungi, mawingu, au kuwa na harufu zaidi
  • Kupata maumivu wakati wa kukojoa
  • au kukojoa mara kwa mara
  • Kuhisi kichefuchefu au kutapika
  • Kupata homa au kuhisi baridi sana n.k

7. Kuwa na tatizo la Lactose intolerance

Mtu mwenye tatizo la lactose intolerance ana shida ya kumeng’enya maziwa na bidhaa zinazotokana na maziwa, kama vile jibini(cheese) na yogurt.

Hii ni kwa sababu hana kiasi cha kutosha cha kimeng’enya(enzyme) kinachoitwa lactase. Lactase huvunja lactose kwenye maziwa, ambayo ina sukari rahisi ya glukosi na galactose.

Watu walio na tatizo la lactose intolerance hawawezi kumeng’enya lactose yote kutoka kwenye chakula na vinywaji. Lactose ambayo haijafyonzwa hupita kwenye utumbo mpana(colon), ambapo bakteria huivunja na kuunda gesi na maji. Ongezeko hili la maji na gesi linaweza kusababisha dalili kama vile:

  • Maumivu ya Tumbo
  • Mtu kuharisha
  • Kuvimbiwa au Tumbo kujaa gesi sana
  • Kuhisi kichefuchefu n.k

8. kuwa na matatizo mengine kama vile vidonda vya tumbo,Crohn’s disease au ulcerative colitis

Crohn’s disease huathiri zaidi utumbo mdogo na ulcerative colitis hutokea kwenye utumbo mkubwa, vyote hivi huweza kusababisha dalili kama vile;

  • Maumivu ya tumbo
  • Kuharisha mara kwa mara
  • Kujisaidia kinyesi kilichochanganyika na damu
  • Mwili kuchoka kupita kiasi n.k

9. Kuwa na tatizo la Constipation

Constipation hutokea wakati mtu hawezi kujisaidia haja kubwa, kupata choo kigumu, au kujisaidia haja kubwa chini ya mara 3 kwa Wiki.

Dalili za tatizo la constipation ni pamoja na:

  • Kupata maumivu ya tumbo
  • Kupata Choo kigumu na kwa shida sana
  • Kupata maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa
  • kujisaidia haja kubwa chini ya mara 3 kwa Wiki.

10. Tatizo la Intestinal obstruction

Wakati hali ya kuziba kwenye utumbo inapotokea chakula hakiwezi kupita kwenye utumbo kama kawaida yake,tatizo hili la kuziba kwa Utumbo kitaalam hujulikana kama Intestinal obstruction

Dalili za tatizo la Intestinal obstruction ni pamoja na:

  • Mtu kupata maumivu makali ya tumbo
  • Mtu kushindwa kujisaidia au kutojisaidia haja kubwa
  • Mtu kuvimba tumbo
  • Mtu kutapika n.k

11. Tatizo la mimba kutunga nje ya kizazi(Ectopic pregnancy)

Kwa wanawake,wakati mwingine maumivu makali ya tumbo upande wa kushoto huweza kutokana na matatizo mbali mbali ya uzazi ikiwemo hili la mimba kutunga nje ya kizazi

Tatizo hili la ectopic pregnancy huweza kutokea ikiwa yai lililorutubishwa hukua nje ya uterasi, kwa kawaida hutokea kwenye mrija wa uzazi au fallopian tube. Mimba inapoendelea kukua inaweza kusababisha kupasuka kwa mirija ya uzazi, hali ambayo inaweza kutishia maisha.

Dalili za mimba kutunga nje ya kizazi ni pamoja na:

  • Mwanamke kupata maumivu ndani ya tumbo au eneo la pelvis
  • Kupata maumivu ya chini ya mgongo
  • Kuvuja damu isiyo ya kawaida ukeni n.k

12. Tatizo la Endometriosis

Endometriosis ni tatizo ambalo linaweza kuathiri wanawake. Tatizo hili hutokea wakati tishu zinapokua nje ya uterasi. Endometriosis huweza kutokea kwa sababu ya matatizo ya mzunguko wa hedhi, sababu za maumbile, au matatizo kwenye mfumo wa kinga mwilini.

Mwanamke mwenye tatizo la endometrosis huweza kupata;

  • Maumivu makali wakati wa hedhi
  • Maumivu ya tumbo
  • Maumivu ya mgongo kwa chini au eneo la Pelvis
  • Maumivu wakati wa tendo au baada ya tendo
  • Maumivu wakati wa hedhi, haja kubwa, au maumivu wakati wa kukojoa n.k

Hizo ndyo baadhi ya sababu zinazopelekea maumivu ya tumbo ikiwemo upande wa kushoto.

KWA USHAURI ZAIDI,ELIMU AU TIBA TUWASILIANE KWA NAMBA +255758286584.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.