Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Takriban watu 795,000 nchini Marekani hufa au kulemazwa kabisa kila mwaka kutokana na utambuzi wa magonjwa usio sahihi #misdiagnosis

FAHAMU:Takriban watu 795,000 nchini Marekani hufa au kulemazwa kabisa kila mwaka kutokana na utambuzi wa magonjwa usio sahihi #misdiagnosis

Na Ugonjwa wa Kiharusi(STROKE) uliongoza kwenye orodha ya matatizo ya kimatibabu ambayo hayajatambuliwa kwa usahihi(misdiagnosed) kisha kusababisha madhara makubwa.

WebMD News Brief
Misdiagnosis Seriously Harms 795,000 People Annually: Study

Takriban Tambuzi 3 kati ya 4 zisizo sahihi (Misdiagnosed Cases) hutokea kwa watu wanaopatwa na mojawapo  ya yale matatizo ambayo hujulikana kama“Big Three” – heart events” kama vile mshtuko wa moyo, maambukizi, au kansa.

Pamoja na kiharusi, magonjwa mengine ambayo husababisha Vifo au ulemavu kwa sababu ya utambuzi usiosahihi(misdiagnosis)ni pamoja na;

  • sepsis(maambukizi ya bacteria kwenye damu)
  • nimonia,
  • kuganda kwa damu kwenye mishipa,
  • Pamoja na saratani ya mapafu.

Kwa wastani, watafiti walikadiria kuwa asilimia 11% ya matatizo ya kiafya husababisha utambuzi mbaya/utambuzi usiosahihi(misdiagnosis), ingawa kiwango cha makosa hutofautiana sana kulingana na ugonjwa huo.

Kiwango cha utambuzi usio sahihi kwa tatizo la mshtuko wa moyo(Heart attack) ni asilimia 1.5% tu, lakini kwa upande wa tatizo la majipu eneo la mgongoni(spinal abscesses) ni asilimia 62%.

Upimaji wa madhara yanayotokea wakati wa utoaji huduma za kitabibu umekuwa eneo gumu la utafiti kutokana na changamoto katika kuandaa takwimu sahihi.

Kwa mujibu wa utafiti uIiyochapishwa Jumatatu katika jarida “BMJ Quality & Safety” utafiti huu wa hivi punde uliunda makadirio kwa kutegemea sana viwango vinavyojulikana vya makosa yanayotokana na magonjwa mahususi.

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.