Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Bima ya Afya Nhif Imekuwa ya Lazima Nyumbani

“NHIF imetimiza miaka 20, wakati tunaanza kilionekana kama ni kitu kigeni kabisa. Kuanzia mwaka wa 2005 kwenda mbele lilianza kuonekana Umuhimu kwahiyo tukaanza kufanya marekebisho ya sheria kuruhusu Makundi mengine tofauti na na watumishi wa umma kuweza kujiunga na mifuko wa Taifa wa Bima ya Afya. Kwahiyo imekuwa ni kitu ambacho ni lazima kuwa nacho nyumbani”. Hipoliti Lello, Meneja Masoko na Huduma kwa Wateja NHIF.

KILICHOBADILIKA NI UTARATIBU WA USAJILI  WA TOTO AFYA KADI

“Awali tulikuwa na Kadi ya Toto Afya kwa utaratibu mwingine lakini tumefanya utaratibu kuanzia Tarehe 13 Machi, 2023 tumebadilisha utaratibu wa kusajili watoto. Hatujafuta lile fao. Tumebadilisha utaratibu wa usajili”

“Mwaka 2015 wakati tunaanzisha lengo letu ni kufikia kila mtoto. Tunajua kwa Sensa ya mwaka 2022 kuna watoto takribani Mil. 31. Hawa watoto wakiwapata wote ina maana umeshatengeneza uhakika wa matibabu kwa kundi hilo la watoto. Tulikuwa tukikatamani watoto wote hao waweze kujiunga na Mfuko”. Hipoliti Lello, Meneja Masoko na Huduma kwa Wateja NHIF.

TUNATAKA MFUKO WA NHIF UWEPO MIAKA MINGI

“Kwa mfano Farhan ana watoto Wawili. Awali huyu mzazi alikuwa akimlipia Mtoto mmoja au Wawili Sh. 50,400 tena wakati mwingine Mtoto akiwa anaumwa Sana ndio anamlipia lakini yeye anasema anajimudu hakuna tatizo.

“Tunapomwambia ajiunge na familia yake maana yake tunataka watu wengi zaidi wajiunge ili kuweza kuchangia kwenye kapu la pamoja. Mmoja wao akipata shida sisi tusiingie gharama ya kumtibia na Mfuko utaendelea kuwa endelevu na uendelee kuwepo na umetimiza miaka 20 sasa uendelee na miaka mingine 50 na 100 na kadhalika”. Hipoliti Lello, Meneja Masoko na Huduma kwa Wateja NHIF

Dr.Ombeni Mkumbwa

Ushauri|Tiba|CheckIn ContactUs; +255758286584 or INBOX. For More Healthtips everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.