Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Figo ya Nguruwe Kufanya kazi katika Mwili wa Binadamu

“Tuna figo ya nguruwe iliyobadilishwa vinasaba ambayo inafanya kazi ipasavyo katika mwili wa binadamu kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa”

Madaktari wa upasuaji nchini Marekani wametangaza kuwa figo ya nguruwe waliyoipandikiza kwenye mwili wa binadamu mgonjwa imefanya kazi ipasavyo kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa, ishara inayotia matumaini katika juhudi za kushughulikia mahitaji makubwa ya utoaji wa viungo.

Madaktari wa upasuaji katika Taasisi ya upandikizaji ya chuo kikuu cha New York walisema Jumatano kwamba hatua muhimu zaidi ni figo ndefu zaidi ya nguruwe kufanya kazi ndani ya mtu.

Wanasayansi wanatumai kuwa upandikizaji wa spishi tofauti unaweza kusaidia kutoa msaada kwa watu wengi ambao wanangojea viungo vinavyoweza kuokoa maisha.

Zaidi ya watu 103,000 nchini Marekani kwa sasa wanahitaji upandikizaji wa viungo, 88,000 kati yao wanahitaji figo.

Maelfu ya watu hufa kila mwaka wakisubiri.

Jamani si hawa wanyama ndio tulifunzwa eti hawana manufaa kwetu
Kumbe ndio watakao tuokoa?

Forum Manager

Content creator&editor (Ms.Asifiwe)Jukumu langu kwako ni kuhakikisha unapata elimu ya kutosha pamoja na Updates mbali mbali ndani ya http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.