Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Kanuni Mpya za Matumizi ya Simu kwa Watoto Wenye Umri Chini ya Miaka 18 -China

Serikali ya China imetangaza kanuni mpya za matumizi ya simu kwa watoto wenye umri chini ya miaka 18.

Kanuni hizo zinaeleza kwamba kwa siku watoto wenye umri kati ya miaka 16 hadi 18 wasitumie simu zaidi ya masaa 2. Pia kanuni hizo zinayataka makampuni ya Internet kuzuia matumizi ya mtandao kuanzia saa 4 usiku  mpaka saa 12 asubuhi. Kwa watoto wenye umri kati ya miaka 8 hadi 16 wao wataruhusiwa kutumia simu kwa saa 1 kwa siku, na kwa watoto chini ya miaka 8 wao wanaruhusiwa kutumia simu kwa muda dakika 8 tu kwa siku.

Tafiti mbalimbali zinaonyesha kwamba matumizi ya simu na vifaa vingine vyenye screen yana athari kwa watoto.

Kwa ujumla wataalamu wanapendekeza kwamba watoto wasitumie simu na vifaa vingine vya simu kwa zaidi ya masaa mawili kwa siku.

China ni nchi ya kwanza kupitisha kanuni za kudhibiti matumizi ya simu kwa watoto…!

Forum Manager

Content creator&editor (Ms.Asifiwe)Jukumu langu kwako ni kuhakikisha unapata elimu ya kutosha pamoja na Updates mbali mbali ndani ya http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.