Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Kenya kuwa miongoni mwa nchi za kwanza kumpokea Mfalme Charles III baadaye mwaka huu

Kenya kuwa miongoni mwa nchi za kwanza kumpokea Mfalme Charles III baadaye mwaka huu:

Kenya itakuwa miongoni mwa nchi za kwanza za Jumuiya ya Madola kumpokea Mfalme Charles III baadaye mwaka huu.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uingereza, safari hiyo itakuwa ni ziara ya kwanza rasmi kufanywa na Mfalme, yenye lengo la kuipa kipaumbele Jumuiya ya Madola wakati wa utawala wake.

Hata hivyo haijulikani ni lini Mfalme Charles III atawasili nchini Kenya, ingawa safari hiyo inatarajiwa kuanza msimu wa vuli.

Mfalme huyo mwenye umri wa miaka 74 alitaka kusherehekea kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa kifo cha mama yake kwa faragha, kwa utulivu na ataungana na mke wake, Malkia Camila.

Ziara hiyo pia itakuwa na kumbukumbu kubwa kwa Mfalme kwani Kenya ndiko mamake, Malkia Elizabeth, alifahamu kifo cha babake Mfalme George IV, na kumfanya mrithi wa kiti cha ufalme.

Malkia Elizabeth, akiandamana na Prince Phillip walikuwa wamezuru Kenya chini ya wiki moja kabla ya habari hiyo, kwa nia ya kuanza ziara ya kuzunguka maeneo mbali mbali ulimwenguni kwa niaba ya mfalme ambaye alikuwa mgonjwa.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.