Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

KENYA:Dereva Ateketea kwa moto na Kufariki Dunia baada ya Gari lake la Mafuta Kugonga Transfoma na kuwaka Moto

Huko Bungoma nchini KENYA,Dereva mmoja Ateketea kwa moto na Kufariki Dunia baada ya Gari lake la Mafuta Kugonga Transfoma na kuwaka Moto,

Lori la kubeba mafuta lililokuwa likisafirisha bidhaa za mafuta liliteketea kwa moto kwenye Barabara Kuu ya Webuye-Malaba asubuhi ya Jumatano, Agosti 9 ‘ Dereva aliyekuwemo aliteketea kiasi cha kutotambulika;

lori hilo lilipogonga transfoma iliyokuwa karibu baada ya kupoteza muelekewo,Wazima moto kutoka serikali ya kaunti ya Bungoma walifika eneo la tukio kuzima moto huo,

Dereva aliyekuwa akiendesha gari la mafuta ya petroli alifariki baada ya kuteketea lori lake liliposhika moto kwenye barabara kuu ya Webuye-Malaba.

Msongamano wa malori mazito kwenye Barabara kuu ya Webuye-Malaba.#Picha:

inaripoti kuwa ajali hiyo ilitokea eneo la Sikata ambapo lori hilo liligonga transfoma ya umeme baada ya Dereva wake kushindwa kulidhibiti.

Madereva wengine walishauriwa kutumia njia mbadala huku wasimamizi wa majanga kaunti wakijitahidi kudhibiti wananchi waliokuwa wamezingira eneo la mkasa.

Kwingineko, TUKO.co.ke iliripoti kuwa mtu mmoja amejeruhiwa baada ya lori la mafuta kulipuka na kushika moto katika soko la Ramula eneo la Gem Kaunti ya Siaya.

Maduka mawili na kituo cha kuuza mafuta yalichomeka katika kisa hicho cha Alhamisi jioni kilichotokea baada ya gari hilo kulipuka. Akithibitisha kisa hicho, Naibu Chifu wa Kata Ndogo ya Ramula Maurice Odine alisema kuwa lori hilo lilikuwa likipakua mafuta katika kituo hicho cha mafuta liliposhika moto ghafla.

Odine aliongeza kuwa moto huo ulisambaa hadi katika maduka mawili yaliyokuwa karibu na kuyateketeza kabisa. Pikipiki tano na gari lililokuwa limeegeshwa katika eneo la mkasa huo pia vililipuka na kuteketea.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.