Kwa Ushauri na Tiba Juu ya Tatizo lolote linalokusumbua TUWASILIANE HAPA.

Bofya hapa
News

Zaidi ya Watu 30 wamefariki kutokana na mafuriko makubwa

Waziri wa Habari wa Somalia, Daud Aweis amesema Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini humo zimesababisha mafuriko makubwa yaliyowaua watu zaidi ya 30.

Aweis amesema watu takribani laki 500,000 wameyahama makazi yao kutokana mafuriko na kuonya kwamba wengine zaidi ya milioni moja huenda wakaathirika.

Uharibifu mkubwa umeshuhudiwa katika mkoa wa Gedo, ulioko kusini mwa Somalia pamoja na Mkoa wa kati wa Hiran ambako kingo za Mto Shabelle zimevunjika na barabara kusombwa na maji katika mji wa Beledweyne.

Taifa hilo la pembe ya afrika limekumbwa na mvua kubwa isiyoisha tangu mwanzoni mwa mwezi Novemba, kutokana na hali ya hewa na ujio wa mvua za El Nino.

DailyStories

Karibu DailyStories Kwa Taarifa Zote Muhimu ndani na Nje. More Updates everyday Link In http://cdp.pvh.mybluehost.me  Also Follow us on Instagram @afyaclass

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.